Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari akimkabidhi Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu tuzo ya kutambua mchango wa NPS katika kufanikisha utekelezaji wa Kliniki za Msaada wa Kisheria nchini, katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za kisheria akiwemo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Julai 13, 2026 Jijini Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Divisheni ya Utaifishaji Mali, Makosa yanayovuka Mipaka na Uhalifu Mahsusi wa NPS Bw. Faraja Nchimbi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili wa Serikali Julai 13, 2026 Jijini Arusha.
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Bi. Bibiana Kileo akipanda mti wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya NPS Urithi wa Kijani uliofanyika tarehe 06 Julai, 2026 Makao Makuu jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu azindua Kampeni ya NPS Urithi wa Kijani uliofanyika tarehe 06 Julai, 2026 Makao Makuu Jijini Dodoma.
Miongozo ya Maamuzi ya Kushtaki, Utaifishaji na Urejeshaji Mali pamoja na Mpango wa Kurejesha, Kutaifisha na Kusimamia Mali imezinduliwa rasmi tarehe 24 Juni, 2026 na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Miongozo ya Maamuzi ya Kushtaki, Utaifishaji na Urejeshaji Mali pamoja na Mpango wa Kurejesha, Kutaifisha na Kusimamia Mali katika hafla iliyofanyika tarehe 24 Juni, 2026.
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha kuhusu matumizi ya taarifa fiche za kifedha katika kufanya uchunguzi sambamba wa kifedha iliyofanyika tarehe 16 na 17 Juni, 2026 jijini Mwanza.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Homera akizindua uwekaji wa jiwe la msingi la Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) Wilaya ya Namtumbo katika hafla iliyofanyika tarehe 11 Mei, 2026 mkoani Ruvuma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Homera akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwenye hafla ya uzinduzi huo uliofanyika tarehe 03 Mei, 2026 Jijini Dar es salaam