Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Historia ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeanzishwa kama Ofisi huru ya Umma kupitia Tangazo la Serikali Na.49 la mwaka 2018 la tarehe 13 Februari, 2018 la kuanzisha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya kutekeleza mamlaka ya Kikatiba aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka ambaye anatoa mchango mkubwa katika kusimamia haki jinai.Kwa mujibu wa Ibara ya 59B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Mkurugenzi wa Mashtaka amepewa uwezo na mamlaka ya kusimamia uendeshaji wa mashtaka yote ya jinai katika Mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi.Kwa msingi huo, Mkurugenzi wa Mashtaka ana uwezo wa kufungua, kuendesha na kusimamia mashtaka yote ya jinai nchini.Kutokana na Ibara hiyo ya Katiba, Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Mashtaka hayamhusu mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine na hawajibiki kusimamiwa na mtu mwingine yoyote au mamlaka nyingine.Katika kutekeleza majukumu yake, Mkurugenzi wa Mashtaka anatakiwa kufuata kanuni zifuatazo:Kutenda haki; Kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria; na maslahi ya umma.Nafasi hii imewekwa chini ya kifungu cha 8 cha Sheria ya Taifa ya Mashtaka, Sura ya 430.

Tangazo la Serikali Na.49 la mwaka 2018 limeweka mpangilio wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, muundo wake, utawala, ufuatiliaji usimamizi wa mashtaka na namna uratibu wa upelelezi utakavyokuwa kwa lengo la kukuza na kuinua utendaji haki jinai na masuala yanayohusiana nayo.