Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Singida

SINGIDA

Mkoa wa Singida una Wilaya tano ambazo ni Singida, Iramba, Manyoni, Mkalama na Ikungi. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Singida ni 2,008,058 huku shughuli za kiuchumi zikiwa ni pamoja na kilimo ambacho huajiri wastani wa asilimia 86 ya wakazi wote. Shughuli nyingine za uzalishaji mali ni ufugaji, uchimbaji wa madini, viwanda vidogo na biashara. Makosa makubwa yanayotendeka katika mkoa huu ni mauaji, ubakaji, dawa za kulevya na nyara za Serikali.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Singida iko Mtaa wa Bomani katikati ya Manispaa ya Singida. Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ina Ofisi katika wilaya ya Manyoni.

 

Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Singida

S. L P 44

Eneo/Mtaa -Bomani \Jengo la Ukaguzi    

Barua pepe:singida@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz