Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Ofisi ya Mashtaka Wilaya ya Nzega
  • Lengo: kutoa huduma za mashtaka kwa umma katika ngazi ya wilaya
  • Majukumu:
  • Majukumu ya Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya ni haya yafuatayo:
  • (i)Kutoa huduma zakimashtaka wilayani ikiwa ni pamoja na kufungua, kuendeshaau kuondoa mashtaka yaliyofunguliwa kwa minajili ya kutenda haki, maslahi ya umma na kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria;
  • (ii)Kuratibu upelelezi na kutoa muongozo kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye makosa ya udanganyifu, rushwa namengine yanayohusiana nayo;
  • (iii)Kuandaa hati za mashtaka, maombi na nyaraka nyingine zinazoendeana na haya;
  • (iv)Kusimamia kesi za rushwa zinazoshughulikiwa na mamlakanyingine zinazopambana na rushwa na udanganyifu;
  • (v)Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi;
  • (vi)Kutoa ushauri kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenyemakosa dhidi ya binadamu na mamlaka za umma;
  • (vii)Kushughulikia kesi zavifo vya mashaka;
  • (viii)Kushughulikiakesi za rufaa na maombi katika mahakama za juu;
  • (ix)Kushughulikia mashahidi kabla, wakati wa kusikiliza kesi na baada ya kutoa ushahidi mahakamani;
  • (x)Kusimamia kesi zinazohusu makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya, ndani ya mamlaka yao;
  • (xi)Kutoa mwongozo,kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika uhalifu na mazalia yake;
  • (xii)Kuratibu kwa kushirikiana na wadau wa haki jinai, kurejesha na kutaifisha mali haramu ndani ya mamlaka yao;
  • (xiii)Kuunganisha ofisi ya mashtaka na taasisi nyingine zinazoendesha mashtaka wilayani kwa lengo la kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwa na mwendesha mashtaka;
  • (xiv)Kufanya ukaguzi sero za polisi na magereza;
  • (xv)Kuwezesha kamati za usimamizi wa uendeshaji kesi katika ngazi ya wilaya na majukwaa mengine;
  • (xvi)Kuandaa na kuchambua data za kesi za jinai;
  • (xvii)Kutunza kanzi data na mfumo wa taarifa wa mashtaka;
  • (xviii)Kuelimisha umma kuhusu uchukuaji na uendeshaji wa mashtaka;
  • (xix)Kutekeleza na kusimamia kanuni za nidhamu za waendesha mashtaka
  • (xx)Kuratibu uchukuaji wa waendeshaji wa mashtaka toka taasisi chunguzi wilayani;
  • (xxi)Kuanzisha na kutunza taarifa za waendesha mashtaka wote wilayani;
  • (xxii)Kuratibu na kuongoza taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya mazingira ,kimtandao na makosa mengine yanayoendana na hayo;
  • (xxiii)Kusimamia kesi za kimazingira na kimtandao zinazoendeshwa na mamlaka nyingine;
  • (xxiv)Kushughulikia maswala ya kiutawala, kifedha nakiutumishi katika mamlaka yao; na
  • (xxv)Kufanya utafiti katika masuala ya jinai na uendeshaji wa kesi zake ili kuhakikisha sheria , kanuni ,amri, taratibu na miongozo yote iliyokwishatolewa inafuatwa.

Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya, itaongozwa na Afisa Mashtaka wa Wilaya