Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Ofisi ya Mashtaka Wilaya ya Temeke

Lengo: kutoa huduma za mashtaka kwa umma katika ngazi ya wilaya

Majukumu:

Majukumu ya Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya ni haya yafuatayo:

(i) Kutoa huduma za kimashtaka wilayani ikiwa ni pamoja na kufungua, kuendesha au kuondoa mashtaka yaliyofunguliwa kwa minajili ya kutenda haki, maslahi ya umma na kuzuia ukiukaji wa taratibu za kisheria;

(ii) Kuratibu upelelezi na kutoa muongozo kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye makosa ya udanganyifu, rushwa na mengine yanayohusiana nayo;

(iii) Kuandaa hati za mashtaka, maombi na nyaraka nyingine zinazoendeana na haya;

(iv) Kusimamia kesi za rushwa zinazoshughulikiwa na mamlaka nyingine zinazopambana na rushwa na udanganyifu;

(v) Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi;

(vi) Kutoa ushauri kwa taasisi zinazotekeleza sheria kwenye makosa dhidi ya binadamu na mamlaka za umma;

(vii) Kushughulikia kesi za vifo vya mashaka;

(viii) Kushughulikia kesi za rufaa na maombi katika mahakama za juu;

(ix) Kushughulikia mashahidi kabla, wakati wa kusikiliza kesi na baada ya kutoa ushahidi mahakamani;

(x) Kusimamia kesi zinazohusu makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya, ndani ya mamlaka yao;

(xi) Kutoa mwongozo, kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika uhalifu na mazalia yake;

(xii) Kuratibu kwa kushirikiana na wadau wa haki jinai, kurejesha na kutaifisha mali haramu ndani ya mamlaka yao;

(xiii) Kuunganisha ofisi ya mashtaka na taasisi nyingine zinazoendesha mashtaka wilayani kwa lengo la kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwa na mwendesha mashtaka;

(xiv) Kufanya ukaguzi sero za polisi na magereza;

(xv) Kuwezesha kamati za usimamizi wa uendeshaji kesi katika ngazi ya wilaya na majukwaa mengine;

(xvi) Kuandaa na kuchambua data za kesi za jinai;

(xvii) Kutunza kanzi data na mfumo wa taarifa wa mashtaka;

(xviii) Kuelimisha umma kuhusu uchukuaji na uendeshaji wa mashtaka;

(xix) Kutekeleza na kusimamia kanuni za nidhamu za waendesha mashtaka

(xx) Kuratibu uchukuaji wa waendeshaji wa mashtaka toka taasisi chunguzi wilayani;

(xxi) Kuanzisha na kutunza taarifa za waendesha mashtaka wote wilayani;

(xxii) Kuratibu na kuongoza taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya mazingira ,kimtandao na makosa mengine yanayoendana na hayo;

(xxiii) Kusimamia kesi za kimazingira na kimtandao zinazoendeshwa na mamlaka nyingine;

(xxiv) Kushughulikia maswala ya kiutawala, kifedha na kiutumishi katika mamlaka yao; na

(xxv) Kufanya utafiti katika masuala ya jinai na uendeshaji wa kesi zake ili kuhakikisha sheria , kanuni ,amri, taratibu na miongozo yote iliyokwishatolewa inafuatwa.

Ofisi ya Mashtaka ya Wilaya, itaongozwa na Afisa Mashtaka wa Wilaya