Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu

Lengo: kutoa utaalamu na huduma za kiutawala na usimamizi wa rasilimali watu katika Ofisi.

Majukumu

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

(i) Kutoa mikakati kwa menejimenti juu ya uendeshaji wa masuala ya Rasilimali watu ikujumuisha masuala ya ajira, uendelezaji wa rasilimali watu, upandishwaji wa vyeo, kutoa motisha, kuweka vivutio vya kazi kwa watumishi ili waendelee kuwepo kwenye Tasisi, kutoa motisha na kudhibiti viwango vya kazi;

(ii) Kuandaa mafao ya mstaafu na likizo kwa watumishi;

(iii) Kuhakikisha uwepo wa tija na ufanisi katika usimamizi na Matumizi ya rasilimaliwatu katika ofisi;

(iv) Kuwa kiungo kati ya ofisi ya taifa ya mashtaka na Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora katika usimamiaji wa Sera na sheria za ajira zinazohusu utumishi wa umma;

(v) Kutoa takwimu za kiutumishi na kuzihuisha; na

(vi) Kukusanya, kuchambua, kuweka na kusambaza takwimu na taarifa zinazohusiana na mipango ya uendelezaji rasilimaliwatu.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na Sehemu mbili (2 ) zifuatazo:

(i) Sehemu ya utawala; na

(ii) Sehemu ya usimamizi wa rasilimali watu.

Sehemu ya Utawala

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

(i) Kutafsiri na kuhakikisha sheria , kanuni za kudumu , machapisho na sheria za kazi zinazohusu utawala na usimamizi wa rasilimaliwatu zinafuatwa;

(ii) Kudumisha mahusiano ya watumishi na maslahi yao ikiwemo afya , usalama , michezo na tamaduni;

(iii) Kutoa huduma za masjala , kumbukumbu za ofisi , huduma za mawasiliano, na utumaji wa nyaraka;

(iv) Kushughulikia masuala ya protokali;

(v) Kuwezesha huduma za utoaji wa ulinzi, usafiri na mahitaji ya kila siku;

(vi) Kuwezesha huduma za uhifadhi ikiwemo matengenezo ya vifaa vya ofisi, majengo na mazingira;

(vii) Kuratibu utekelezaji na ukuzaji wa maadili na masuala muhimu katika utumishi wa umma;

(viii) Kutekeleza masuala ya mtambuka ikiwemo jinsia , ulemavu, ukimwi na magonjwa yasiyoambukizwa na masuala ya mazingira;

(ix) Kuratibu utekelezaji wa uboreshaji wa mifumo ya utendaji kazi;

(x) Kushauri juu ufanisi wa utendaji wa ofisi;

(xi) Kuratibu maandalizi/utekelezaji wa mkataba wa huduma kwa wateja; na

(xii) Kuratibu utekelezaji wa ushirikishwaji wa sekta binafsi;

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

Sehemu ya usimamizi wa rasilimaliwatu

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

(i) Kuratibu masuala ya ajira, kupangia vituo vya kazi, kuthibitishwa kazini, kupandishwa vyeo na uhamisho kwa watumishi;

(ii) Kuwezesha mafunzo na ukuaji wa maendeleo ya kazi (maendeleo ya kitaaluma, kukuza ujuzi, kukuza utendaji wa kazi na maandalizi ya kustaafu);

(iii) Kuratibu mafunzo kazi kwa ajili ya waajiriwa wapya katika utumishi wa umma;

(iv) Kuandaa na kutekeleza mipango ya rasilimaliwatu na maendeleo;

(v) Kusimamia mishahara na malipo;

(vi) Kuandaa na kuboresha kumbukumbu za watumishi ikiwa ni pamoja na likizo za mwaka, kustaafu, ugonjwa, uzazi na masomo;

(vii) Kuandaa maslahi na stahili za watumishi;

(viii) Kuratibu utekelezaji wa upimaji kazi wa wazi kwa watumishi;

(ix) Kuandaa makisio ya ikama ya watumishi na bajeti kwa kila mwaka;

(x) Kuandaa na kuwezesha utekelezaji wa mpango wa kurithishana madaraka; na

(xi) Kuanzisha na kuratibu mafunzo ya ndani na ya kazi kwa watumishi;

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.