Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Mwanza
Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Mwanza
MKOA-MWANZA
Mkoa wa Mwanza unapakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa Viktoria liko kaskazini. Mkoa wa Mwanza una idadi ya watu 3,699,872 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na makazi ya mwaka 2022 likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 19,592.
Shughuli kuu za Kiuchumi katika Mkoa huu ni Kilimo, ufugaji, uvuvi, madini, utalii, viwanda na biashara. Makosa makubwa yanayojiri katika Mkoa huo ni Mauaji, Ubakaji, Ulawiti, Uvuvi haramu, na Wizi
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Mwanza iko katikati ya Jiji la Mwanza Mtaa wa Nyamagana.
Anwani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Mwanza
S. L P 331
Eneo/Mtaa -Nyamagana
Barua pepe:mwanza@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz