Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Dodoma

MKOA-DODOMA.

Mkoa wa Dodoma una wilaya tano ambazo ni Dodoma, Kondoa Mpwapwa, Kongwa Mpwapwa na Bahi. Mkoa wa Dodoma una jumla ya eneo la ardhi la kilomita za mraba 41311. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, mkoa una jumla ya watu wapatao 3,085,625. Pia, makosa yanayotendeka kwa kiasi kikubwa katika mkoa huu ni mauaji na ukatili wa kijinsia.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Dodoma imeanzishwa mwaka 1971 wakati huo ikiwa chini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo mwaka 2018 ikarejea rasmi kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) ikiwa katika jengo la Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Dodoma.  Kwa upande wa Wilaya, Ofisi ya Taifa ya Mashtakta mpaka sasa imefungua ofisi za mashtaka katika wilaya nne ambazo ni Kondoa, Mpwapwa, Chemba na Kongwa.

 

Anuani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Dodoma  

S. L P 963

Eneo/Mtaa -NSSF House 

Simu:  026-2321889

Barua pepe:dodoma@nps.go.tz

Tovuti: www.nps.go.tz