Kitengo cha Huduma za Utafiti na Maktaba
Lengo: kutoa utaalamu na huduma katika utafiti wa kisheria, huduma za uchapishaji na maktaba.
Majukumu:
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
(i) Kufanya utafiti wa kisheria katika uendeshaji wa mashtaka na masuala yanayohusiana nayo;
(ii) Kuwajulisha watumiaji wa maktaba kuhusu bidhaa mpya za sheria;
(iii) Kuwekea maktaba vifaa vya kutosha vya utafiti, nyenzo na nyaraka za rejea;
(iv) Kuweka katika maktaba katiba, sheria na nyaraka mbali mbali za kisheria;
(v) Kutunza vitabu vya rejea vya kesi, machapisho na majarida ya kisheria na magazeti;
(vi) Kutunza rejesta ya machapisho ya rejea;
(vii) Kuwezesha uazimaji wa machapisho ya rejea;
(viii) Kuanzisha mfumo wa ubadilishanaji wa sheria zinazohusiana na uendeshaji wa mashtaka na kazi kutoka nchi zilizo katika jumuiya ya madola na zisizo za jumuiya; na
(ix) Kushauri juu ya ununuzi wa machapisho ya kisheria.
Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa Mkuu wa Maktaba.