Kitengo cha TEHAMA
Kitengo cha TEHAMA
Lengo: kutoa utaalamu na huduma kwa matumizi ya TEHAMA ;
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
(i) Kutekeleza mpango mkakati wa TEHAMA na Serikali Mtandao;
(ii) Kuendeleza na kuratibu mifumo TEHAMA kwa kushirikiana na wakala ya serikali mtandao;.
(iii) Kuhakikisha kwamba vifaa na programu za TEHAMA zinasimamiwa na kutunzwa
(iv) Kuratibu na kutoa msaada katika ununuzi wa programu na vifaa vya TEHAMA;
(v) Kuanzisha na kuratibu matumizi ya mawasiliano ya barua pepe na mitandao;
(vi) Kufuatilia na kusimamia usalama wa mifumo ya mawasiliano na taarifa; na
(vii) Kufanya tafiti na kushauri juu ya matumizi ya tehama kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma.
Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa TEHAMA Mkuu.