Kitengo cha Uhasibu na Fedha
Lengo: kutoa huduma za usimamizi wa kifedha na utunzaji wa vitabu vya vitabu vya kihasibu.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
Mishahara
(i)Kuandaa malipo ya mishahara ikiwemo makato yaliyoainishwa kisheria;
(ii)Usimamizi wa mishahara;
(iii)Kuandaa taarifaza pensheni; na
(iv)Kutunza kumbukumbu.
Ofisi ya Fedha
(i)Kuwasilisha orodha ya malipo hazina;
(ii)Kuweka fedha na kuwasilisha hundi benki;
(iii)Kuandaa ripoti ya kila mwezi;
(iv)Kulipa fedha/hundi kwa wafanyakazi na wateja (watoa huduma);
(v)Kulipa malipo ya jumla;
(vi)Kutunza vitabu vya fedha;
(vii)Kurekodi na kuhakiki masurufu yaliyotolewa; na
(viii)Kuandaa na kufanya malipo.
Mapato
(i)Kusimamia mapato kulingana na kanuni na miongozo;
(ii)Kukusanya kodi ya kila mwaka,ada za maombi na vyanzo vingine;
(iii)Kusimamia na kukusanya mapato; na
(iv)Usuluhishi wa kibenki.
Pensheni
(i)Kuandaa nyarakaza pensheni; na
(ii)Kutunza kumbukumbu za pensheni.
Bajeti
(i)Usimamizi wa bajeti;
(ii)Kufuatilia ugawaji na matumizi ya fedha;
(iii)Kuandaa taarifa za mwisho na taarifa nyingine za kifedha.
Uhakiki na ukaguzi wa awali
(i) Kuhakiki na kupitisha nyaraka za malipo kwa mujibu wa kanuni;
(ii) Kuhakiki nyaraka za kifedha kwa mujibu sheria, kanuni na miongozo
inayosimamia fedha za umma; na
(iii)Kutoa majibu kwa hoja za ukaguzi
Kitengo kitaongozwa na Mhasibu Mkuu.