Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Lengo: kutoa utaalamu na huduma za habari, mawasiliano , mazungumzo na umma pamoja na vyombo vya habari.
Kitengo hiki kitakuwa na majukumu yafuatayo:
(i) Kupata na kusambaza taarifa kwaajili ya kuhabarisha umma juu ya sera, programu kazi na maboresho yanayofanyika;
(ii) Kuratibu utoaji wa taarifa kwenye vyombo habari;
(iii) Kufanya mazungumzo na umma pamoja na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu ofisi;
(iv) Kuratibu maandalizi ya nyaraka za kisekta;
(v) Kuratibu maandalizi na uzalishaji wa makala za ofisi katika magazeti na majarida; na
(vi) Kuhuisha taarifa za kisekta kwenye tovuti.
Kitengo hiki kitaongozwa na Afisa Habari Mkuu.