Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Divisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji Fedha na Rushwa

Lengo: kutoa utaalamu na huduma ya mashtaka kwa makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha, rushwa, mazingira na mali asili.

Majukumu

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 • (i)Kupitia na kutoa ushauri kwenye sera. Sheria, kanuni , miongozo na viwango katika usimamizi wa makosa ya udanganyifu , utakatishaji fedhana rushwa;
 • (ii)Kuratibu kesi za rushwa katika mahakama kuu kitengo cha makosa ya rushwa na uhujumu uchumi na mahakama za chini;
 • (iii)Kuratibu taasisi zinazotekeleza sheria katikamakosa ya udanganyifu,utakatishaji fedha,rushwa na masuala yanayohusiana nayo;
 • (iv)Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za udanganyifu na rushwa katika ngazi za mikoa na wilaya;
 • (v)Kufungua na kuendesha kesi za rushwa na udanganyifu;
 • (vi)Kusimamia mapitio ya majalada ya kesi za utakatishaji fedha, rushwa na udanganyifu;
 • (vii)Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja nawadau katika kupambana na makosa ya udanganyifu , utakatishaji fedha na rushwa;
 • (viii)Kusimamia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa ya udanganyifu, utakatishaji fedha na rushwa; na
 • (ix)Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na rushwa na udanganyifu.
 • Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu (3) kama ifuatavyo:
 • (i)Sehemu ya makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha;
 • (ii)Sehemu ya makosa ya rushwa; na
 • (iii)Sehemu ya mazingira na mali asili.
 • Sehemu ya makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha
 • Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
 • (i)Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na viwango katika usimamizi wa kesi za udanganyifu na utakatishaji fedha na kupendekeza maboresho;
 • (ii)Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza sheria katika masuala yanayohusiana na makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha na yanayohusiana nayo;
 • (iii)Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha katika ngazi za mikoa na wilaya;
 • (iv)Kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na makosa ya rushwa na udanganyifu;
 • (v)Kusimamia na kushauri uendeshaji wa kesi za makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha ili kuleta tija;
 • (vi)Kufanya mapitio ya majalada kutoka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosaya udanganyifu na utakatishaji fedha;
 • (vii)Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa , kimataifa na kikanda pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya udanganyifu na utakatishaji fedha; na
 • (viii)Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosaya udanganyifu na utakatishaji fedha.
 • Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.
 • Sehemu ya Makosa ya Rushwa
 • Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
 • (i)Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni,Miongozo na viwango katika usimamizi wa kesi za rushwa na kupendekeza maboresho;
 • (ii)Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya rushwa na yanayohusiana nayo;
 • (iii)Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za rushwa na yanayohusiana nayo katika ngazi ya mkoa na wilaya;
 • (iv)Kufungua na kuendesha kesi za rushwa na masuala yanayohusiana nayo;
 • (v)Kusimamia na kushauri njia bora za uendeshaji wa kesi za rushwa;
 • (vi)Kufanya mapitio ya majalada kutoka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana makosa ya rushwa;
 • (vii)Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya rushwa; na
 • (viii)Kushughulikia rufaa na maombi ya kesi za rushwa.
 • Sehemuhii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.
 • Sehemu ya Makosa ya Mazingira na Maliasili
 • Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
 • (i)Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni,Miongozo na viwango katika usimamizi wa kesi za mazingira na mali asili na kupendekeza maboresho;
 • (ii)Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya mazingira na mali asili;
 • (iii)Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za mali asili na mazingira;
 • (iv)Kusimamia na kufuatilia kesi za mazingira na mali asili zinazoendeshwa na taasisi nyingine;
 • (v)Kusimamiamapitio ya majalada ya kesi za mazingira na mali asili kutoka vyombo chunguzi;
 • (vi)Kuratibu ushirikiano na mashirika yakimataifa na kikanda pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya mazingira na mali asili; na
 • (vii)Kushughulikia rufaa na maombi ya kesi za mali asili na mazingira.
 • Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.