Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Divisheni ya Utaifishaji Mali, Makosa yanayovuka Mipaka na Uhalifu Mahsusi

Lengo: kutoa utaalamu na huduma ya kunyang’anya wahalifu au washirika wao faida zitokanazo na vitendo vya uhalifu pamoja na kuendesha kesi hizo mahakamani.

Majukumu

Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 • (i)Kuratibu utekelezaji wa sheria pamoja na masuala yote yahusuyo utaifishaji na urejeshajimali zitokanazo na uhalifu;
 • (ii)Kufuatilia na kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi zinazohusiana na utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika kutenda uhalifu na mazalia yake;
 • (iii)Kuratibu tathmini ya ufanisi wa sheria, kanuni, miongozo na viwango kwenye masuala ya utaifishaji na urejeshaji mali zitokanazo na uhalifu na kupendekeza marekebisho yake;
 • (iv)Kuratibu utambuzi na ufuatiliaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifuna mazalia yake;
 • (v)Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kimataifa na kikanda katika ufuatiliaji, utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake;
 • (vi)Kufuatilia na kusimamia utambuzi wa kesi zenye uwezekano wa kuwa na mali za kurejesha;
 • (vii)Kufuatilia na kusimamia mali zilizozuiliwa, taifishwa na kurejeshwa;
 • (viii)Kutoa ushauri na muongozo kuhusu maombi ya utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake, yanayoombwa kwa au najamhuri ya muungano wa tanzania;
 • (ix)Kuratibu,kutathimini na kushauri ufanisi wa sera, sheria, kanuni,miongozo na viwango vya usimamizi wa makosa yanayovuka mipaka na kupangwa;
 • (x)Kuratibu na kutoa miongozo kwa mamlaka zinazotekeleza sheria katika masuala yahusuyo makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
 • (xi)Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi zamakosa yanayovuka mipaka na kupangwa katika ngazi zamikoa na wilaya;
 • (xii)Kufunguana kuendesha kesi za makosa yanayovuka mipaka, ya kupangwa na masuala yanayohusiana nayo;
 • (xiii)Kusimamia mapitio ya majalada yanayohusiana na makosa yanayovuka mipakana ya kupangwa toka vyombo chunguzi;
 • (xiv)Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikandapamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
 • (xv)Kuratibu na kusimamia masuala yanayohusuubadilishanaji wa wahalifu watoro kama itakavyoelekezwa na waziri mwenye dhamana na masuala ya sheria;
 • (xvi)Kushauri kwenye masuala ya ushirikianowa kesi za jinai;
 • (xvii)Kusimamia uendeshaji wa kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa;
 • (xviii)Kuwezesha uhudhuriaji wa mashahidi kutoka na kwenda nje ya nchikutoa ushahidi;
 • (xix)Kuratibu na kutoa miongozo kwa mamlaka zinazotekeleza sheria katika masuala ya makosa ya kimtandao;
 • (xx)Kuratibu ushirikiano na mashirika ya kitaifa, kimataifa na kikandapamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya kimtandao; na
 • (xxi)Kuratibu na kushauri ufanisi katika uendeshaji wa kesi za makosa ya kimtandao.

Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na Sehemu tatu (3) kama ifuatavyo:

 • (i)Sehemu ya utaifishaji na urejeshajimali;
 • (ii)Sehemu ya Makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa; na
 • (iii)Sehemu ya Makosa ya kimtandao.

2.1.1.1.2.1Sehemu ya Utaifishaji na Urejeshaji Mali

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 • (i)Kusimamia utekelezaji wa Sheria za utaifishaji na urejeshaji mali pamojana masuala mengine yanayohusiana nayo;
 • (ii)Kutathmini na kushauri ufanisi wa Sheria, Kanuni, Miongozo na viwango kwenye masuala ya utaifishaji na urejeshaji mali zitokanazo na uhalifu na kupendekeza marekebisho yake;
 • (iii)Kusimamia utambuzi wa kesi zenye uwezekano wa kuwa na mali za kurejesha;
 • (iv)Kufungua na kuendesha kesi zinazohusu utaifishajina urejeshajimali ndani na nje yanchi;
 • (v)Kusimamia utambuzi na ufuatiliaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake;
 • (vi)Kushirikiana na mashirika ya kimataifa na kikanda katika ufuatiliaji,utaifishaji na urejeshaji wa zana zinazotumika katika kutenda uhalifu na mazalia yake;
 • (vii)Kusimamia utekelezaji wa sheria za utaifishaji na urejeshajimali pamoja masuala yanayohusiana nayo;
 • (viii)Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa sheria, Kanuni, Miongozo na viwango katika utekelezaji wa amri za utaifishaji na urejeshaji mali na kupendekeza marekebisho;
 • (ix)Kusimamia utekelezaji wa amri za uzuiaji na utaifishaji mali pamoja na wadau wa urejeshaji mali;
 • (x)Kushirikiana na mashirika ya kimataifa na kikanda katika utekelezaji wa amri za utaifishaji na urejeshaji mali;
 • (xi)Kusimamiamali zilizozuiliwa, taifishwa na kurejeshwa;
 • (xii)Kushauri juu ya uondoshaji na ugawanyaji wa mali zilizotaifishwa;
 • (xiii)Kuandaana kutunza kumbukumbu za mali zote zilizo shikiliwa, zuiliwa, taifishwa na kurejeshwa; na
 • (xiv)Kutathmini mali zilizozuiliwa, taifishwa na kurejeshwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.2.2Sehemu ya Makosa yanayovuka mipaka na ya kupangwa

Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:

 • (i)Kutathmini na kushauri kuhusiana na ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni,Miongozo na viwango katika usimamizi wa kesi za madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia na kupendekeza marekebisho;
 • (ii)Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza Sheria kwenye masuala yanayohusiana na makosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia;
 • (iii)Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia pamoja na masuala yanayohusiana nayo katika ngazi za mikoa na wilaya;
 • (iv)Kufungua na kuendesha kesi za makosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia pamoja na masuala yanayohusiana nayo.
 • (v)Kusimamia na kushauri uendeshaji wa kesi zamadawa ya kulevya,ugaidi na uharamia ili kuleta tija;
 • (vi)Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia;
 • (vii)Kutoa ushauri na maoni ya kisheria kwa taasisi za kimataifa na mamlaka zinazoshughulikiamakosa ya madawa ya kulevya, ugaidi na uharamia;
 • (viii)Kutathmini na kushauri ufanisi wa Sera, Sheria, Kanuni, Miongozo na Viwango katika usimamizi wamakosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinaina kupendekeza marekebisho;
 • (ix)Kuwasiliana na taasisi nyingine zinazotekeleza sheria katika masuala yanayohusiana na usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi zajinai kulingana na Sheria na taratibu husika;
 • (x)Kufungua na kuendesha kesi zinazohusiana na usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinai kulingana na Sheria na taratibu husika;
 • (xi)Kusimamia na kushauriuendeshaji wa kesi za usafirishaji haramu wa binadamu ili kuleta tija;
 • (xii)Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinai;
 • (xiii)Kuwasiliana na taasisi za kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na wadau katika masuala ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikianokatika kesi za jinai;
 • (xiv)Kutoa ushauri na maoni ya kisheria kwa taasisi za kimataifa na mamlaka zinazoshughulikia makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, ubadilishanaji wa wahalifu na ushirikiano katika kesi za jinai;
 • (xv)Kushughulikia na kushauri kuhusu ushirikiano katika kesi za jinai pale ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaomba au inaombwa na mamlaka za nchi nyingine;
 • (xvi)Kushughulikia masuala yanayohusiana na wahalifu watoro, uhamishaji wa wafungwa na kutafuta mashahidi; na
 • (xvii)Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na utwaaji wa wahalifu.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

2.1.1.1.2.3Sehemu ya Makosa ya Kimtandao

Sehemu hii itafanya kazi zifuatazo:

 • (i)Kutathmini na kutoa ushaurikuhusiana na ufanisi waSera, Sheria, Kanuni, Miongozo na viwango katika usimamizi wa makosa ya kimtandao na kupendekeza marekebisho;
 • (ii)Kuwasiliana na taasisi zinazotekeleza sheria za makosa ya kimtandao na yale yanayohusiana nayo;
 • (iii)Kufuatilia ufunguaji na uendeshaji wa kesi za makosa ya kimtandao katika ngazi ya mikoa na wilaya;
 • (iv)Kufunguana kuendesha kesi za makosa ya kimtandao;
 • (v)Kusimamia na kutoaushauri wa uendeshaji wa kesi za makosa ya kimtandao kwa ufanisi;
 • (vi)Kufanya mapitio ya majalada toka vyombo chunguzi na kutoa maelekezo stahiki kuhusiana na makosa ya kimtandao;
 • (vii)Kuwasiliana na taasisi za kitaifa, kimataifa na kikanda pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya makosa ya kimtandao;kna
 • (viii)Kushughulikia kesi za rufaa na maombi yanayohusiana na makosa yakimtandao.

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.