Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Divisheni ya Kusimamia Uendeshaji Mashtaka.
 •  
 • Lengo: kutoa ushauri wa kitaalamu na huduma za uendeshaji mashtaka nchini.
 •  
 • Majukumu:
 • Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
 • (i)Kuratibu utekelezaji wa programu ya uendeshaji wa mashtaka;
 • (ii)Kuratibu na kuandaa miongozo inayohusu upelelezi na uendeshaji kesi za jinai;
 • (iii)Kusimamia ukaguzi, ufatiliaji na ubora wa hudumazinazotolewa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka;
 • (iv)Kufuatilia na kutathiminiutekelezaji wa miongozo inayotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka kuhusiana na upelelezi na uendeshaji mashtaka ya jinai;
 • (v)Kuratibu upelelezi ili kuhakikisha ufanisi katika upelelezi unaoratibiwaa na mwendesha mashtaka
 • (vi)Kuratibu na kusimamia matumizi bora ya mwongozo wa waendesha Mashtaka na Mwongozo wa Wapelelezi;
 • (vii)Kuandaa mahitaji ya mafunzo ya kisheria ili kuleta tija katika mashtaka;
 • (viii)Kuratibu ukaguzi wa sero za polisi na magereza;
 • (ix)Kuratibu ufuatiliaji wa majukumu waliyopangiwa kwa watumishi na maafisa wengine ndani ya taasisi;
 • (x)Kutafuta ufumbuzi wa masuala ya kisheria yanayotokana na maamuzi ya mahakama ambayo yanahitaji utekelezaji wa wadau wengine;
 • (xi)Kushirikisha wadauwa haki jinai katikamasuala ya kesi za jinai;
 • (xii)Kuratibu ukusanyaji wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kuhusiana na kesi zinazoendelea au kuishaili kuleta tija katika uendeshaji wa kesi za jinai;
 • (xiii)Kuratibu uchambuzi wa taarifa zilizokusanywa;
 • (xiv)Kuratibu ukusanyaji taarifa za mashauri ya jinai,kuchambua kitakwimu ili kupata taarifa zitakazosaidia kuleta tija katika mashtaka na hivyo kupunguza makosa ya jinai;
 • (xv)Kufungua , kuendesha na kusimamiamashtaka na
 • (xvi)Kusimamia rufaa na maombi ya jinai mahakamani kwa niaba ya Jamhuri.
 •  
 • Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itakuwa na sehemu tatu (3) zifuatazo:
 • (i)Sehemu ya uendeshaji mashtaka;
 • (ii)Sehemu ya usimamizi wamashtaka mahakamani; na
 • (iii)Sehemu ya makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa Taifa.
 •  
 • 2.1.1.1.1.1 Sehemu ya Uendeshaji mashtaka
 •  
 • Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
 • (i)Kuratibu utekelezaji wa programu ya uendeshaji mashtaka;
 • (ii)Kuandaa miongozo ya uendeshajiwa mashtaka;
 • (iii)Kufuatilia na kutathiminiutekelezaji wa miongozo inayotolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka kuhusiana na upelelezi na uendeshaji mashtaka ya jinai;
 • (iv)Kuandaa na kutunza kanzi data ya waendesha mashtaka na mawakili wa serikali;
 • (v)Kuratibu na kusimamia mipango na upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya programu ya uendeshaji mashtaka;
 • (vi)Kuratibuutwaaji wa uendeshaji mashtaka toka vyombo chunguzinchini;
 • (vii)Kuhabarisha umma kuhusu masuala ya uendeshaji mashtaka;
 • (viii)Kuratibu na kushauri sera,sheria,kanuni,miongozo na viwango katika kushughulikia makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (ix)Kuratibu kesi zinazohusiana na makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (x)Kuratibu utekelezaji wa sheria katika vyombo vinavyotekeleza sheria vinavyohusu makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (xi)Kuratibu ushirikiano wa kitaifa,kimataifa na kikanda na wadau wengine katika mapambano dhidi ya makosa ya binadamu na utengamano wa taifa na
 • (xii)Kuratibu masuala yanayohusiana na mkanganyiko washeriaza ukatili wa kijinsia nawatoto.
 • Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.
 •  
 • 2.1.1.1.1.2 Sehemu ya Menejimenti ya Mashtaka
 •  
 • Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
 • (i)Kufuatilia, kukusanya na kuchambua taarifa za kesi zinazoendelea na zilizoisha ili kuelewa muundo na tabia za kesi;
 • (ii)Kukusanya na kuchambua taarifa za kesi za wakosaji wa pekee na washirika wao kwa lengo la kusimamia na kupata taarifa za kiintelejensia zitakazowezesha uendeshaji bora wa mashtaka nchini;
 • (iii)Kuratibu ukusanyaji taarifa za mashauri ya jinai, kuzichambua kitakwimu ili kupata taarifa zitakazosaidia kuleta tija katika uendeshaji wamashtaka;
 • (iv)Kuanzisha na kutunza kanzi data ya taarifa za kiintelejensia;
 • (v)Kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa za kiintelijensia na maafisawanaoshughulikia kesiili kuweza kuandaa mfumo wakieletroniki wakesi (casedocket) na uendeshaji wakemahakamani; na
 • (vi)Kuwezesha ubadilishanaji wa taarifa za kiintelijensia na wadau wengine ili kupunguza uhalifu na hivyo kudumisha amani na usalama wa nchi

Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.

 •  
 • 2.1.1.1.1.3 Sehemu ya makosa dhidi ya Binadamu na Utengamano wa Taifa.
 •  
 • Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
 • (i)Kupitia na kushauri kuhusu sera, sheria ,kanuni, miongozo na viwango katika kusimamia mashauri ya makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (ii)Kusimamiakesi dhidi ya binadamu na utengamano wa kitaifa;
 • (iii)Kusimamia vyombo vinavyotekeleza sheria katika mapambano dhidi ya makosa ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (iv)Kufuatiliauanzishaji na uendeshaji wa kesi za makosadhidi ya binadamu na utengamano wa taifa na yanayohusiana na hayo katika ngazi ya mkoa na wilaya;
 • (v)Kufungua na kuendesha kesi za makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa kitaifa na yanayohusiana nayo;
 • (vi)Kusimamia ufunguaji na uendeshaji wa kesi zamakosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (vii)Kusimamia mapitio ya majalada yanayohusiana na makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (viii)Kuwasiliana na mashirika ya kitaifa,kimataifa na kikanda pamoja na wadau wengine katika mapambanoya makosadhidi ya binadamu na utengamano wa taifa;
 • (ix)Kusimamia chunguzi za vifo vya mashaka;
 • (x)Kushauri kuhusu namna bora ya kutunza amani ,usalama na utulivu wa nchi;
 • (xi)Kushughulikiamasuala yoteyanayohusu mkanganyiko wa sheria dhidi ya ukatili wa jinsia na watoto.
 • (xii)Kusimamia rufaa na maombi mbalimbali mahakamani yanayohusu makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa; na.
 • (xiii)Kushughulikia rufaa na maombi mbalimbali ya kesi za makosa dhidi ya binadamu na utengamano wa taifa.
 •  
 • Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi.