Wanawake watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wakisherekea Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa tarehe 8 Machi, 2023.
Mjumbe wa Tume ya Rais ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi akifungua kikao cha Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Tume ya Mhe. Rais juu ya uboreshaji wa mfumo wa Haki Jinai kilichofanyika Jijini Dodoma
Washiriki wa Kikao kazi cha Menejimenti na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa wakifuatilia mada mbalimbali zinazowasilishwa kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika tarehe 13 hadi 14 Februari, 2023 Jijini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha Menejimenti na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa walioshiriki kwenye kikao kazi kilichofanyika tarehe 13 hadi 14 Februari, 2023 Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu (katikati)) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka walioshiriki kwenye Kikao kazi cha Menejimenti na Wakuu wa Mashtaka wa Mikoa kinachofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 14 Februari, 2023 Makao Makuu Jijini Dodoma.
Washiriki wa kikao kazi cha Uandaaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu Nusu Mwaka 2022/2023, Re-allocation na Maoteo ya Bajeti 2022/2023 wakifuatilia hotuba ya Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Joseph Pande wakati akihutubia kwenye kikao kazi hicho kinachofanyika Jijini Arusha
Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka washiriki maandamano ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika tarehe 22 Januari, 2023 Jijini Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka washiriki kwenye maandamano ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika tarehe 22.01.2023 Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylivester Mwakitalu akisalimiana na uongozi wa Gereza Kuu la Butimba jijini Mwanza wakati wa Ziara maalumu ya kutembelea Magereza Nchini tarehe 27.12.2022