Ofisi ya Mashtaka ya Mkoa wa Iringa
. MKOA-IRINGA.
Mkoa wa Iringa uko katika nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Mkoa huu una eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 58,936. Iringa ina hifadhi mbili za Taifa ambazo ni Ruaha na Udzungwa. Pia kuna hifadhi za misitu pamoja na maeneo yaliyohifadhiwa, mashamba ya misitu. Idadi ya watu katika Mkoa wa Iringa ni 1,192,728, kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022. Shughuli kuu za kiuchumi katika Mkoa wa Iringa ni Kilimo, ufugaji, viwanda, biashara na utalii.
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika Mkoa wa Iringa iko katikati ya Manispaa ya Iringa. Kwa upande wa kupeleka huduma za mashtaka wilayani, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tayari imefanikwa kufungua ofisi katika wilaya zote tatu za Mkoa wa Iringa ambazo ni Mufindi, Kilolo. Makosa makubwa yanayojiri kwa kiasi kikubwa katika Mkoa huu ni Ubakaji, Ulawiti na Ujangili.
Anuani -Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Iringa
S. L P 2401
Eneo/Mtaa -Boma
Barua pepe:iringa@nps.go.tz
Tovuti: www.nps.go.tz