Divisheni ya Mipango
Lengo:kutoa utaalamu katika maeneo ya mipango, utekelezaji wa bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
Majukumu
Divisheni hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
(i) Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa mipango na bajeti;
(ii) Kuratibu maandalizi ya michango kwenye hotuba ya bajeti ya waziri na ripoti ya kila mwaka ya uchumi;
(iii) Kuratibu maandalizi, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya maendeleo;
(iv) Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa miradi programu za maendeleo na ukusanyaji wa rasimali zinazohitajika;
(v) Kuandaa, kutekeleza na kuboresha mpango wa usimamizi wa vihatarishi;
(vi) Kuandaa rejesta ya vihatarishi; na
(vii) Kutoa mwongozo na ushauri ili kuhakikisha kuwa vihatarishi vinatambuliwa, tathminiwa na kupunguzwa.
Divisheni hii itaongozwa na Mkurugenzi na itajumuisha Sehemu mbili (2) zifuatazo: -
(i) Sehemu ya mipango na bajeti; na
(ii) Sehemu ya ufuatiliaji na tathmini.
Sehemu ya mipango na bajeti.
Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
(i) Kuratibu uandaaji wa mpango kazi wa mwaka, kati na mpango mkakati;
(ii) Kuainisha miradi ,programu,mipango kazi na kuendeleza mikakati ya ukusanyaji wa rasilimali;
(iii) Kushirikiana na wizara ya Katiba na Sheria ,Wizara ya fedha na Uchumi katika uandaaji wa mpango mkakati na bajeti;
(iv) Kutoa msaada wa kiufundi katika mchakato wa kuandaa mpango mkakati na bajeti; na
(v) Kuandaa maandiko na makubaliano ya miradi na programu kwa ajili ya kupata rasilimali fedha za ndani na nje ya nchi;
Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi
Sehemu ya ufuatiliaji na tathimini
Sehemu hii itakuwa na majukumu yafuatayo:
(i) Kufatilia utekelezaji mpango kazi wa mwaka na mpango mkakati;
(ii) Kuandaa ripoti za utekelezaji;
(iii) Kuandaa ripoti ya uendeshaji mashtaka nchini;
(iv) Kutoa michango katika maandalizi ya mipango ya kitaifa ,programu na masuala ya kibajeti ikiwemo uanishaji wa malengo na viashiria vya utendaji;
(v) Kutoa misaada ya kiufundi katika kusimika mifumo ya tathimini na ufuatiliaji;
(vi) Kufanya utafiti na tathmini juu ya matokeo za mipango,miradi na programu;
(vii) Kukusanya maoni ya wadau kuhusiana na huduma zinazotolewa;
(viii) Kuratibu utekelezaji wa mwaka na nusu mwaka;
(ix) Kuandaa , kutekeleza na kuhuisha mpango wa usimamizi wa vihatarishi;
(x) Kuandaa na kusimamia rejesta ya vihatarishi; na
(xi) Kutoa mwongozo na ushauri ili kuhakikisha kuwa vihatarishi vinatambuliwa, tathminiwa na kupunguzwa.
Sehemu hii itaongozwa na Mkurugenzi Msaidizi