Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

ZINGATIENI MAADILI YA UTUMISHI KWENYE MAENEO YENU YA KAZI
03 Feb, 2021
ZINGATIENI MAADILI YA UTUMISHI KWENYE MAENEO YENU YA KAZI

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makalloamewasihi watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuzingatia Maadili katika maeneo yao ya kazi pamoja na kufanya kazi kwa bidii.

Naibu Mkurugenzi Makallo ameyasema hayo mapema leo wakati akifungua mafunzo ya ukusanyaji, uchakataji, utumiaji na utunzaji wa takwimu za kesi za Jinai na kumbukumbuza makosa ya Rushwa kwa Makatibu Sheria wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yanayofanyika Mkoani Singida kuanzia tarehe 03 Februari 2021.hadi tarehe 08Februari,2021

Bw. Makallo amesema kada ya utumishi wa Makatibu wa Sheria inakumbana na changamoto mbalimbali za kiutendaji na kimaadilihivyo mafunzo hayo wanayopatiwa yatumike kuwasaidia na kuboresha utendaji wao wa kazi.

Amesema katika miaka ya karibuni dunia imeshuhudia kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanadamu kiuchumi,kijamii, kisiasa, kiteknolojia na kiutamaduni ambapo athari za mabadilikohayo ni pamoja na kubadilika kwa mbinu za kupanga na kutekeleza uhalifu na hivyo kuwataka Makatibu wa Sheria wakiwa ni miongoni mwa watoa huduma katika taasisi ya Haki Jinai kukumbuka kuwa wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanashiriki katika kupambana na kuzuia uhalifu huo kwa njia ya kutekeleza vema majukumu yao.

Aidha, amesema kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imejipanga vyema katika kushughulikia matendo ya mmomonyoko wa maadili kwa watumishi wa Umma ambapo hatua madhubuti zimekuwa zikichukuliwa kwa watumishi wanaobainika kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Amesema watumishi wa Umma wakizingatia miiko iliyopo katika utendaji wao wa kila siku huleta matokeo chanya kwa huduma wanazotoa kwa jamii na hivyo jamiu hujenga imani kwa serikali na kuleta hali ya Usalama.

Bw. Makallo alitoa rai kwa Makatibu Sheria waliohudhuria mafunzo hayokuwa kila aliyepata mafunzo arudipo katika sehemu yake ya kazikuweka ujuzi aliopata kwa vitendo na kushirikisha ujuzi walioupata kwa wengineambao hawajapata nafasi ya kuhudhuria mafunzo ili kupanua ushiriki wa mafunzo wa Makatibu Sheria wengi zaidi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutunza siri zinazohusu taarifa za majalada yanayowafikiahuku wakielewa kwamba suala la utunzaji wa siri ni la lazima kwa watumishi wote wa Umma.

Mafunzo hayo ya siku sita kwa Makatibu Sheriayameandaliwa kwa ushirikiano wa Divisheni ya Usimamizi wa Kesi na Uratibu wa UpelelezinaDivisheni ya Makosa ya Udanganyifu, Utakatishaji Fedha na Rushwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Katika mafunzo hayo mada mbalimbalizitatolewa zikiwepo mada juu ya Maadili ya Makatibu Sheria, Kutunza na kushughulikia majalada ya rushwa, ukusanyaji, uchakataji na utumaji wa takwimu za kesi, utunzaji na mfumo wa regista ya ofisi,mfumo wa kielektroniki wa upokeaji na utunzaji wa majalada, utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka za serikali pamoja na.masuala mengine yanayohusu maadili.