WATUMISHI WA NPS WAHIMIZWA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Sylvester Mwakitalu, amewahimiza watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) kushiriki katika shughuli za uwekezaji na za kijamii ili kuimarisha ustawi wao, kujenga ushirikiano na kuongeza ufanisi kazini.
Bw. Mwakitalu ametoa wito huo Novemba 20, 2026, wakati akizungumza katika kikao cha kawaida cha Baraza la Wafanyakazi la NPS kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Akizungumzia umuhimu wa kushiriki katika shughuli za kijamii, amewahimiza watumishi kudumisha mahusiano mema na kujenga utamaduni wa kusaidiana. Ameeleza kuwa mahusiano hayo huimarisha mawasiliano na ushirikiano kazini, hivyo kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya pamoja.
Bw. Mwakitalu amewahimiza watumishi kutumia fursa za kiuchumi na elimu ya uwekezaji wanayoipata mara kwa mara ili kuongeza kipato na kuimarisha ustawi wao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Sambamba na hayo, DPP Mwakitalu pia amesisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu kwa weledi, uadilifu na uwajibikaji. Akiongeza kuwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ni msingi wa kuwapatia wananchi huduma bora za mashtaka kwa wakati.
