Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
14 Dec, 2020
WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA

Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma Wilaya ya Kasulu katika kesi Na.32/2020 mbele ya Mhe. Jaji A. Matuma imewatia hatiani washtakiwa Enock Antony pamoja na baba yake Antony Kinanila na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua kwa makusudi Cosmas Pastory.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 26, Desemba 2018 katika Kijiji cha Katundu Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa walimuua marehemu kwasababu ya mgogoro wa ardhi na kwamba marehemu alikuwa anajidai kuwa yeye ni tajiri. Washtakiwa walienda kwa marehemu usiku wakamkuta amekaa nje ya nyumba yake na familia yake ndipo wakamkamata, wakamlaza chini chali kisha wakamchoma mkuki kifuani mbele ya familia yake.

Kesi hiyo imeendeshwa na Mawakili wa Serikali Robert Magige na Edna Makala.