Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Wafungwa miaka thelathini jela kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya
09 Nov, 2020
Wafungwa miaka thelathini jela kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya

Mahakama Kuu ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Dar es Salaam katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 14/2918 mbele ya Mhe. Jaji Banzi imewatia hatiani washtakiwa Nabibarkhshsh Pribakhsh na Mohamaddhanif Nazirahmad Dorzade kwa kosa la kupatikana na Madawa ya Kulevya aina ya Heroin Hydrochloride kiasi cha Kilogramu 111.2 na Gramu 451.7 za Bangi na kuwahukumu kwenda jela kifungo cha miaka thelathini pamoja na kutaifisha jahazi ambalo walitumia kutenda kosa hilo

Shauri hili limeendeshwa na Mawakili wa Serikali Monica Mbogo, Cecilia Shelly, Batilda Mushi na Clara Charwe

Aidha, mahakama imewaachia huru watuhumiwa kumi na moja (11) katika kesi hiyo ambao majina yao ni

Abdullah Khatoon Sahib,

Ubeidulla Gulamzade Abdi, Naim Baltik Ishqa

Moslem Amiree Golmohamad,

Rashid Badfar, Omary Dorzade Ayoub, Tahir Bishkar Mubarak,

.Abdulmajid Asqan Pirmuhamad,

Ally Abdallah Ally,

Juma Amour Juma,

Omari Saidi Mtangi.

Mbele ya Mh Jaji Banzi. Mahakama imemtia hatiani Nabibarkhsh Pribakhsh na Mohamaddhanif Nazirahmad Dorzade

ambao walikuwa ni miongoni mwa washtakiwa katika shauri hilo. Hata hivyo upande wa Mashtaka haujaridhishwa na Maamuzi ya Mahakama ya kuwaachia huru Washtakiwa hao na umekata rufaa kupinga hukumu hiyo.