UONGOZI WA NPS WAJIPANGA KUONGEZA UFANISI WA UTENDAJI KAZI
Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mashtaka, Bw. Sylvester Mwakitalu, imejipanga kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya taasisi kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za mashtaka na kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati.
Akizungumza wakati wa kufungua Kikao Kazi cha Menejimenti cha Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Fedha 2026/2027, kilichofanyika tarehe 15 hadi 16 Oktoba 2026 jijini Dar es Salaam, Bw. Mwakitalu amesisitiza umuhimu wa viongozi kusimamia kwa karibu utekelezaji wa majukumu katika Divisheni na Vitengo vyao ili kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, katika kikao hicho ziliwasilishwa taarifa za utekelezaji wa majukumu kutoka kwa Wakuu wa Divisheni na Vitengo, zilizobainisha shughuli zilizotekelezwa katika kipindi husika pamoja na matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli hizo. Uwasilishaji wa taarifa hizo umelenga kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa majukumu, kuimarisha usimamizi wa rasilimali za taasisi pamoja na kuweka mikakati ya kutatua changamoto zinazojitokeza katika utendaji kazi.
Kikao hicho kimehitimishwa kwa Menejimenti kuazimia kuendelea kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa majukumu ya Divisheni na Vitengo kuanzia ngazi za Wilaya na Mikoa yote ya Kimashtaka nchini ili kuongeza uwajibikaji na kuendeleza matumizi ya teknolojia katika kuboresha mifumo ya utendaji kazi. Hatua hizo zinatarajiwa kuchangia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya NPS na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi.
