Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Kahama
07 Sep, 2020
Ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Kahama

Naibu katibu mkuu wa wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju amezindua rasmi Ofisi yaTaifa ya Mashtaka Wilayani Kahama ikiwa ni lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.

Amesema kuwa uwepo wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itasaidia kupnuguza kero kwa wananchi waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo hususani mjini Shinyanga

Katika hatua nyingine Mpanju amesema ziara waliyofanya ya kutemebelea Magereza katika Mkoa wa Shinyanga alibaini kuwa washitakiwa wengi ni wale wanaokabiliwa na makosa ya Mauaji yatokanayo na Ramri chonganishi na kusababisha migogoro ya kifamilia na kuvuruga amani ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Mganga amebainisha kuwa baada ya kutembelea Magereza hayo ameamuwa kuwafutia Mashtaka washitakiwa 147 katika Mkoa waShinyangaambao walikuwa wakisubiri kesi zao kutajwa Mahakamani na kuwataka kwenda kuwa raia wema.

Biswalo ameongeza kuwa katika ufutaji wa mashtaka hayo wamezingatia vigezo vikuu viwilivinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria ambavyo ni pamoja Maslahi ya taifa na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha katika mashauri hayo.

Amesema kuwa miongoni makosa yaliyofutwa kwa washtakiwa ni pamoja na makosa ya Mauaji, kupigana, kukamatwa na gongo,na kuingia na kufanya uvamizi kwenye migodi bila ya kuwa na vibali maalum

Awali akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga Naibu Msajili wa Mahakama kuu Kanda hiyoRamli Mbuya amesema kuwa Wilaya ya Kahama yenye Halmashauri tatu za Msalala,Ushetu na Kahama Mjini zina matukio mengi ya Uhalifu ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa huo.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali Mkoa wa Shinyanga Bi Magreth Ndaweka amesema kuwa awali wananchi walipaswa kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 100 kufuata hudumahizo mjini Shinyanga hali iliyokuwa ikichangia mashauri mengi kuchelewa kusikilizwa hivyo uanzishwaji wa ofisi ya mashtaka wilaya ya Kahama utakuwa sehemu ya kupunguza malalamiko na Msongamano Magerezani.

Mmoja wa wakazi wa Mji wa Kahama aliyeshuhudia kufunguliwa kwa huduma za kimashtaka katika eneo hiloWilfred Birago ameipongeza Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuona umuhimu na uhitaji wa huduma hiyo na kuamua kuwasogezea kwani walikuwa wakiitafuta umbali mrefu hali iliyokuwa ikichangia haki kuchelewa kutolewa