Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

RAIS SAMIA AMWAPISHA BIBIANA KILEO KUWA NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA
29 Apr, 2024
RAIS SAMIA AMWAPISHA BIBIANA KILEO KUWA NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  tarehe 28 Aprili, 2024 amewaapisha Viongozi watatu katika nyadhifa mbalimbali, akiwemo Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo.

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika katika Ikulu ya Magogoni Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi wengine wakuu wa Kitaifa, akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.

Wengine ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Hassan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Dkt. Moses Kusiluka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi na wengine wengi.

Viongozi wengine walioapishwa ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria ambae ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Winfrida Korosso na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali,  Bi. Alice Mtulo.

Waapishwa hao waliteuliwa na Rais Samia kushika nyadhifa hizo tarehe 4 Aprili, 2024. Kabla ya uteuzi huo, Bi. Bibiana alikuwa Mkuu wa Mashtaka wa Mkoa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mwanza na Bi. Alice alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Kesi na Udhibiti wa Ubora katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.