Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Rais Magufuli apongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kazi nzuri inazozifanya
25 Aug, 2020
Rais Magufuli apongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kazi nzuri inazozifanya

Rais Magufuli ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka chini ya uongozi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Bw. Biswalo Mganga kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha mali ya Serikali haipotei.

“Ofisi ya DPP wamefanya kazi nzuri, wamesimamia mali ya Serikali na kuhakikisha haipotei. DPPhakikisha unafikisha pongezi kwenye Ofisi yako. Mmefanya kazi nzuri sana . Ahsanteni kwa utendaji bora. “ Alipongeza Mhe. Rais Magufuli baada ya kukagua magari yaliyotaifishwa kutokana na makosa mbalimbali ya Uhujumu Uchumi.

Mhe. Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo tarehe 25 Agosti, 2020 baada ya kukagua magari 132 yaliyotaifishwayakiwepo malori na magari madogo baada ya magari hayo kutumika katika matukio ya Uhujumu Uchumi yakiwepo matukio ya rushwa, upatu, utakatishaji fedha na madawa ya kulevya ambapo baada ya kukamatwa yalihifadhiwa katika Kituo cha Mabasi cha zamani jijini Dodoma.

Mhe. Rais alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama likiwepo jeshi la polisi kuendelea kuchapa kazi na kuhakikisha wanawashika wale wote wanaohujumu uchumi. “endeleeni kuchapa kazi, endeleeni kulinda maeneo ya mipakani, wanaotorosha fedha wakamatwe” alisisitiza Mhe. Raisambapo pia aliwapongeza Wananchi wote wanaoshiriki kutoa taarifakwakuwa wanaisaidia serikali kutekeleza majukumu yake vizuri.

Baada ya kukagua magari yaliyotaifishwa Mhe. Rais aliagiza magari hayo yawe yamegaiwa kwa taasisi mbalimbali za serikali ndani ya wiki mbili kuanzia tarehe 25 Agosti, 2020 ili yasaidie katika utendaji kazi na kutoa huduma kwa wananchi.

Akitoa taarifa kwa Mhe. Rais Naibu Mkurugenzi wa MashtakaBw. Edson Makallo alisema magari yaliyotaifishwa yanatokana na kesi zilizoendeshwa mahakamani kati ya mwaka 2011/2012 na kuishana baada ya serikali kushinda kesi hizo ilipewa ruhusa ya kutaifishamali.