Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA YATOA MSAADA GEREZA KUU ISANGA - DODOMA
03 Jul, 2024
OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA YATOA MSAADA GEREZA KUU ISANGA - DODOMA

Wakili wa Serikali Mwandamizi Bi. Pamela Shinyambala kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu akikabidhi vifaa mbalimbali vikiwepo Mifuko ya Saruji 80, Sinki za choo 10 pamoja na Tanki za choo 10 kwa Mkuu wa Gereza Kuu Isanga Kamishna Msaidizi wa Magereza Zefania Elias Neligwa.

Msaada huo umetolewa leo tarehe 3 Julai, 2024 na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma kufuatia maombi yaliyotolewa na Wafungwa na Mahabusu wakati wa ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu pamoja na wadau wengine wa Haki Jinai walipotembelea Gereza Kuu Isanga mnamo tarehe 12 Juni, 2024 Jijini Dodoma.

Aidha ACP Neligwa ameshukuru kwa niaba ya Kamishna Generali wa Magereza kwa ushirikiano na msaada uliotolewa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuguswa na maisha ya wafungwa na mahabusu waliopo katika gereza hilo.