NPS YASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), ikiongozwa na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Bi. Bibiana Kileo, imeshiriki uzinduzi rasmi wa Awamu ya Pili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign) uliofanyika katika Viwanja vya Dole, Kizimbani, Zanzibar, Juni 20, 2026.
Kampeni hiyo imezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye amesema kuwa utekelezaji wa kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuboresha huduma za sheria na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Katika kuunga mkono jitihada hizo, mawakili wa Serikali kutoka NPS wanatoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi katika viwanja hivyo, kwa lengo la kuhakikisha wananchi, hususan wasiokuwa na uwezo, wanapata haki kwa wakati na kwa ufanisi.
