Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

"Niwapongeze watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kazi nzuri mnayoifanya" NAIBU WAZIRI MHE. JUMANNE SAGINI
05 Jun, 2024
"Niwapongeze watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kazi nzuri mnayoifanya" NAIBU WAZIRI MHE. JUMANNE SAGINI

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kazi nzuri wanaiyofanya katika uendeshaji wa mashauri ya Jinai. 

"Mashauri tunayoshinda ni mengi kuliko tunayofeli kinyume na ilivyokuwa hapo awali. Kuwepo kwa ofisi hii imeonyesha tija iliyo bayana."

Naibu Waziri amebainisha hayo wakati alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu Jijini Dodoma tarehe 04 Juni, 2024 na kuzungumza na Watumishi wa ofisi hiyo.

Sambamba na hilo Mhe. Naibu Waziri amewataka watumishi hao kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kikatiba ili kuiwezesha nchi kwenda mbele na uhalifu uweze kupungua.

Pia Mhe. Jumanne ameagiza watumishi hao kuweka kipau mbele cha mafunzo ili kuweza kuwasaidia kuongeza ujuzi katika makosa ya jinai hususani katika masuala ya kiusalama ya kimtandao.

"Msisite kutoa elimu kwa wale ambao wanakwamisha kazi zenu. Wakati mnajenga uwezo wenu wale wadau wenu mnaoona wanahitaji kupata elimu ni vizuri mkajumuika nao ili kuimarisha umoja." Amebainisha hayo Mhe. Sagini.