Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAPONGEZA WATUMISHI WA OFISI YA TAIFA MASHTAKA MKOA WA ARUSHA
08 May, 2024
NAIBU MKURUGENZI WA MASHTAKA AWAPONGEZA WATUMISHI WA OFISI YA TAIFA MASHTAKA MKOA WA ARUSHA

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka  amewapongeza watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Arusha kwa kazi nzuri wanayoifanya katika  Uendeshaji wa Mashauri ya Jinai katika mkoa huo na  kuwataka kuendelea na moyo huo wa kujitoa kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa mshikamano ili kutimiza malengo ya Taasisi.

Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo wakati alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Arusha mara baada ya kumaliza kushiriki  kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika tarehe 1 Mei, 2024 Jijini Arusha.

"Kwa niaba ya timu nzima ya Menejimenti ninaahidi tutaendelea kupambana usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba maslahi ya watumishi wote wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka yanaboreshwa na pia kuhakikisha kwamba mipango yote ya Taasisi tuliyonayo yanafikiwa." Amebainisha hayo Naibu Mkurugenzi Bibiana.