Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MWENYEKITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA NA TIMU YAKE WATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA.
15 Feb, 2023
MWENYEKITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA NA TIMU YAKE WATEMBELEA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala  Bora Jaji Mstaafu Mhe. Mathew Mwaimu akiwa ameongozana na Makamishna wa Tume ya  Haki za Binadamu na Utawala Bora wametembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa lengo la kujenga ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Makamishna wa Tume hiyo wamepata nafasi ya kuzungumza na wajumbe wa menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kikao kifupi kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka jijini Dodoma.

Mwenyekiti huyo wa Tume alitumia nafasi hiyo kutoa elimu juu ya majukumu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  na kuainisha maeneo ambayo Tume hiyo na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wanaweza kushirikiana katika utendaji kazi.

Naye Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu alimshukuru Mwenyekiti huyo wa Tume ya  Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuitembelea Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na kuahidi kwamba Ofisi ya Taifa ya Mashtaka itashirikiana na Tume hiyo.

Ziara ya Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwenye Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imefanyika jijini Dodoma tarehe 14 Februari, 2023.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni wadau muhimu katika utoaji Haki.