Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MKUU WA MKOA AMEWATAKA WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI KUFANYA KAZI KWA WELEDI
05 Mar, 2022
MKUU WA MKOA AMEWATAKA WAENDESHA MASHTAKA NA WAPELELEZI KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Mkuu Wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Mhandisi Robert Gabriel aliwataka Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kufanya kazi kwa weledi na ubunifu katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.

Akifunga mafunzo kwa Waendesha Mashtaka na Wapelelezi kutoka katika Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini yaliyofanyika jijini Mwanza kuanzia tarehe 28 Februari hadi 4 Machi,2022 yaliyohusu taratibu za Kisheria ya Utaifishaji Mali na Makubaliano ya Kukiri Makosa alisema elimu na ujuzi watakayoipata yatawasaidia kutekekeza kwa ukamilifu majukumu yao na kupunguza msongamano wa mahabusu mahakamani.

Alisema wahalifu wanatumia mbinu mbalimbali katika kufanya Uhalifu hivyo kushiriki kwenye mafunzo ni muhimu ili kuendana na mbinu mpya za kupambana na Uhalifu.

"Nalinganisha tukio hili la mafunzo na kazi mkata kuni ambapo ili kuweza kukata kuni vizuri ni vizuri kulinoa shoka".

Aliyasema hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Akizunguza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu aliwashukuru Majaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ambao walikuwa ni Sehemu ya Wakufunzi kwa kukubali kufika kutoa mada licha ya majukumu makubwa waliyonayo wakati huu wa kuanza kwa Mwaka Mpya wa Mahakama.

Aliwataka washiriki wa mafunzo kuonyesha matokeo ya mafunzo waliyopewa kuleta matokeo na mabadiliko yenye tija katika utendaji wao wa kazi.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la PAMS Bw. Samson Kassala aliwapongeza washiriki kwa moyo wa kujitoa na kuzingatia mafunzo waliyopewa ambapo aliahidi Shirika la PAMS kuendelea kuiunga mkono Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kudhamini shughuli mbalimbali na kuliletea taifa Tija.

Naye Bw.Paul Kadushi ambaye ni Mkurugenzi wa Divisheni ya Utaifishaji Mali, Makosa ya Kupangwa na Uhalifu Mahsusi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka alisema Malengo makuu ya mafunzo ni kuwajengea uwezo Waendesha Mashtaka na Wapelelezi katika kuboresha utendaji wa kazi.