Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw Biswalo Mganga ,aliongoza timu ya Mawakili wa Serikali .
31 Mar, 2020
 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw Biswalo Mganga ,aliongoza timu ya Mawakili wa  Serikali .

Mnamo tarehe 30 Machi, 2020 Mkurugenzi wa Mashtaka nchini,aliongoza timu ya Mawakili waSerikali bwana Shadrack Kimaro ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Utaifishaji wa mali zitokanazo na Uhalifu na Wakili wa Serikali Mwandamizi bwana Chiristopher Msigwa kuwasilisisha hoja za Jamhuri katika Shauri la Maombi ya kutaifisha jumla ya Shilingi za kitanzaniaBilioni kumi na sita , million miasaba ishirin, laki nane na hamsini na nane elfu mia tano sabini na tisa na senti arobaini na saba (16,720,858,579.47) ambazo ni mazalia ya uhalifu unaotokana na Mchezo wa Upatu ambao unaokatazwa kisheria .

Maombi hayo yalisikilizwa mbele ya Mheshimiwa Jaji E.Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa. Imekuwa ni kawaida kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kuinuka yeye mwenyewe na kwenda Mahakamani kuendesha kesi akiambatana na Mawakili wa Serikali.Utaratibu huu ni mzuri kwa kuwa unawajengea Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kujiamini zaidi.

Mahakama kwa upande wake imepangam kutoa uamuzi dhidi ya maombi hayo mnamo tarehe 3 April,2020.