Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yakabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
22 Sep, 2020
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yakabidhi vifaa vya TEHAMA kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imepokea msaada wa Printa Tano na Skana Sita kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania uliokabidhiwa Jijini Dodoma leo na Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka hiyo Bw. Joannes Karungura kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo.

Akikabidhi vifaa hivyoMkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Bw. Johannes Karungura kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka alisema lengo la msaada huo ni kuwezesha Serikalina wadau waweze kuwa na uelewawa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Akipokea vifaa hivyo Mkurugenzi wa MashtakaBw. Biswalo Mgangakwa niaba ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuipatia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka vifaa hivyo na kueleza kwamba vitasaidia kwenda na maendeleo ya teknolojia.

“Tumekuwa tunafungua Ofisi vifaa hakuna havitoshelezi, msaada huu utatusaidia sana tuendelee kushirikiana kwa ajili ya kusaidia nchi yetu”, alisema Bw. Mganga

Naye Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Edson Makallo alitumia fursa hiyo kuishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa msaada walioutoa akieleza kwamba kushukuru ni kuomba tena na kuwataka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wanapopata vifaa vingine waendelee kusaidia.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Sheusi Mburi nae pia aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kueleza kuwa msaada huo utasaidia kupunguza tatizo la uhaba wa vifaa vya TEHAMA na kuwataka wanapopata nafasi nyingine ya kusaidia waweze kufanya hivyo.

Naye Mkurugenzi wa ugavi na manunuzi Bw. Jimmy Nathani Ntimaza aliishukuru ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na kueleza kuwakwa kutupatia msaada wa vifaa hivyo itasaidia kuchangia kupunguza manunuzi ya vifaa kwa kutumia njia ya manunuzi ya kawaida ya kiofisi kwani inakuwa na mlolongo mkubwa na kutumia muda mrefu kwa manunuzi hayo ya vifaa vya ofisi.

Hii ni awamu ya pili ya msaada wa vifaa vya TEHAMA kutoka Mamlaka ya MawasilianoTanzaniakwa Ofisi ya TaifaMashtaka ambapo mara ya kwanza walitoa msaada wa Tarakilishi (Kompyuta) 20, na Printa 10 vyenye thamani ya Sh. Milioni 62.