Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MAKAMU WA RAIS KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA ARINSA
28 Aug, 2019
MAKAMU WA RAIS KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA ARINSA

MAKAMU WA RAIS KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA ARINSA NA MKUTANO MKUU

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza maadhimisho ya Miaka 10 ya Umoja wa Taasisi zinazokabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kutumia dhana ya utaifishaji na urejeshaji mali zitumikazo au kutokana na uhalifu kwa nchi za Kusini mwa bara la ambao kwa kiingereza unafahamika kama ‘Asset Recovery Inter-Agency Network for Southern Africa (ARINSA).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Augustine Mahiga amesema maadhimisho hayo yatakayofanyika Jijini Dar es salaaam katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano cha Julius Nyerere yatahudhuriwa na baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Wakurugenzi wa Mashtaka, Wakuu wa Taasisi za Upelelezi pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka katika nchi wanachama 16 wa ARINSA.

"Maadhimisho haya, yatafanyika Jijini Dar es salaaam katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano cha Julius Nyerere, yanatarajiwa kuhudhuriwa na baadhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Wakurugenzi wa Mashtaka, Wakuu wa Taasisi za Upelelezi pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka katika nchi wanachama 16 wa ARINSA," alisema Mhe.Mahiga

Amesema umoja huo ulianzishwa ili kuwa na ushirikiano wa karibu wa kitaasisi baina ya nchi wanachama kwa lengo la kuhakikisha kuwa wahalifu hawafaidiki na mali zinazohusiana na uhalifu