Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MAHABUSU 72 WAFUTIWA MASHTAKA
02 Dec, 2020
MAHABUSU 72 WAFUTIWA MASHTAKA

Jumla ya Mahabusu Sabini na mbili kati yao wanaume 62 na wanawake 10 wamefutiwa Mashtaka na Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga baada ya kutembelea gereza la Karanga, Moshi kujionea hali halisi ya gereza pamoja na kuwasikiliza mahabusu


Mkurugenzi wa Mashtaka amefanya tukio hilo leo baada ya kukagua na kujionea hali halisi ya gereza hilo ambapo alipata pia nafasi ya kuwasilikiliza wafungwa na Mahabusu.
Akizungumza baada ya kuwafutia Mashtaka Mahabusu hao Bwana Mganga aliwataka watakaporudi uraiani kuwa raia wema na wale wanaobaki gerezani kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu ili awasamehe dhambi walizotenda na kufungua mlango wa rehema.


Aidha aliwaonya kutorudia kufanya Uhalifu. "Sitegemei kuwakuta mmefanya Uhalifu tena baada ya kutoka hapa, ole wenu mrudie. Kama kuna miongoni mwenu ambaye anajua hawezi kuacha Uhalifu aombe abaki humu ndani" Alisisitiza Bw. Mganga


Mkurugenzi wa Mashtaka alitumia nafasi hiyo kuwaonya watu wanaotishia mashahidi na wanaotaka kupata haki kwa njia ya Udanganyifu kwakuwa akikamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.


Katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Mashtaka aliahidi kuchukua changamoto zilizotolewa na Mahabusu na wafungwa na kuahidi kuzifanyia kazi.


Mkurugenzi wa Mashtaka na timu ya viongozi kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wapo katika Mikoa mbalimbali kukagua namna shughuli za uendeshaji wa shughuli za Mashtaka unavyotekelezwa ikiwapo kutembelea Magereza, mahabusu na kuwatembelea wadau muhimu wanaoshirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Haki Jinai.