Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

MAAFISA TRA NA BENKI WALIOACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA KISUTU WATIWA HATIANI KWA KOSA LA UTAKATISHAJI FEDHA
19 Aug, 2022
MAAFISA TRA NA BENKI WALIOACHIWA HURU NA MAHAKAMA YA KISUTU WATIWA HATIANI KWA KOSA LA UTAKATISHAJI FEDHA

Mahakama ya Rufani imetoa hati ya kuwakamata na kuwaweka rumande washtakiwa wanne, akiwamo aliyekuwa mfanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Idara ya wafanyabiashara wakubwa anaefahamika kwa jina la Justice Katiti.

Awali, wajibu rufani walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi ya jinai namba 152 ya mwaka 2010 kwa mashtaka kumi, yakiwamo kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Washtakiwa hao wanadaiwa kula njama ya kufanya uhalifu, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya Udanganyifu kiasi cha shilingi milioni 338 na utakatishaji fedha haramu.

Mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao, baada ya kutengua uamuzi wa hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu Kanda ya Dar es salaam ya kuwaachia huru washtakiwa hao, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Mbali na Katiti, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya rufani ya Namba 15/2018 ni Robert Mbetwa na Gidion Otullo, waliokuwa wafanyabiashara na Godwin Paula. Na jopo la Majaji watatu wa Mahakama hiyo, wakiongozwa na Shabani Lila, Ignas Kitusi na Lilian Mashaka, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Katika uamuzi huo, jopo hilo la majaji limeamuru wajibu rufani wawekwe mahabusu huku jalada la kesi hiyo, likielezwa kurejeshwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kutoa adhabu.

Awali, jopo la Mawakili wa Serikali Waandamizi watatu likiongozwa na Nassoro Katuga, Hellen Moshi na Tumaini Mafuru, walidai Serikali ilikata rufaa baada ya kutoridhika na hukumu iliyotolewa Mahakama ya Kisutu na Mahakama Kuu.