Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Kitilya na wenzake kulipa bilioni 1.5
27 Aug, 2020
Kitilya na wenzake kulipa bilioni 1.5

Mkurugenzi wa MashtakaBw. Biswalo Mgangaamewafutia mashtaka 57Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushauri wa Uwekezaji, Huduma za Uwezeshaji na Upatikanaji wa Fedha Harry Kitillya na wenzake wanne baada ya makubalianona kuwabakizia shtaka mojala kuisababishiaSerikali hasara ya Dola Milioni Sitakatika kesi ya Uhujumu Uchumi inayowakabili.Kitillya na wenzake wanne wameamuriwa kulipa fidia ya Tsh. 1.5 Bilioni na faini ya shilingi milionimoja.

Kitilya ambaye ni Kamishana Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato( TRA) na wenzake wametakiwa kulipa fidia na faini hiyo kwenye Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kwa kosa la kuisababishia Serikali hasara ya Dola milioni Sita.

Washtakiwa hao wamehukumiwa adhabu hiyo baada ya kukiri makosa yao katika kesi iliyokuwa ikiwakabili walipofanya majadiliano na upande wa mashtaka. Washitakiwa hao wakikamilisha kulipa faini hiyo watarejea uraiani baada ya kukaa mahabusu kwa miaka minne na miezi minne wakati kesi yao iliyobakia ikiendelea kusikilizwa.

Akitoa adhabu hiyo juzi Jaji Emmaculate Banzi alisema amezingatia mawasilaino ya hoja za mashtaka na maelezo ya upande wa utetezi. Mbali na Kitillya washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana.

Akiwakilisha hati mpya ya Mashtaka yenye shtaka moja,Wakili waSerikali MkuuOswald Tibabyekomaaliwasomeawashitakiwa maelezo ya mashtaka yao akielezea hatua kwa hatua jinsi walivyojipangana kufanikisha kosa hilo kisha Jaji Banzi aliwauliza washtakiwa iwapowamesikiliza mashataka hayo, washtakiwa wote walikubalina ndipo wakatiwa hatiani.

Baada ya washtakiwa kutiwa hatiani, Mkurugenzi wa shtaka Biswalo Mgangaaliiomba makahakama iwaamuru kulipa fidia ya shilingi Bilioni 1.5 kwa hasara waliyoisababishia Serikalikwa mujibu wa Mkataba wa makubalianowaliyoyafanya .Wakili Alex Mgongolwa aliyekuwa akiwatetea washitakiwa hao aliiomba mahakamaiwaonee hurumana iwape adhanu ndogokwakuwa wamekiri makosa na hivyo kuokoa muda wa mahakamana rasilimali fedha.

Kitillya na wenzakewalikuwa mahabusu tangu Aprili Mosi, 2016 walipopandishwa kizimbanikwa mara ya kwanzakatikaMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kukamilisha hatua za awali kwani mashataka ya utakatishaji fedha hayana dhamana.