Habari

Imewekwa: Jul, 22 2022

KIKOSI KAZI CHA ULINZI KWA WATOTO DHIDI YA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINADAMU CHAZINDULIWA

News Images

Waziri Wa Katiba naSheria Mhe. DamasNdumbaroamezindua kikosi kazi cha ulinzi kwa watoto dhidi ya biashara haramu ya Usafirishaji wa binadamu.

Kikosi kazi hicho kimeanzishwa chini ya Mradi wa kupambana na Uhalifu mkubwa wa kupangwa ( Serious Organised Crime- SOC), ambacho kitatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizindua kikosi kazi hicho, Waziri wa Katiba na Sheria, leo Julai 21, 2022 Dkt. Damas Ndumbaro, amesema athari ya uhalifu mkubwa wa kupangwa ni kubwa na inakuwa ya kushtukiza.

"Sisi, Tanzania tunayo mifano hai kuhusu madhara ya uhalifu wa aina hii, kwa mfano uripuaji wa mabomu katika ubalozi wa Marekani uliotekelezwa hapa kwetu, Kenya na Uganda kwa wakati mmoja." Amesema Dkt.Ndumbaro na kuongeza

Amesema kutokana na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali katika mapambano dhidi ya ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto, wameanza kushuhudia kuibuka kwa taarifa kuhusu uhalifu wa aina hiyo katika jamii na umeonesha bayana juu ya kazi kubwa iliyopo katika kukabiliana na janga hilo.

" Kwa maelezo hayo ninajenga hoja kwamba mradi huu wa kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa hasa ule wa usafirishaji haramu wa Binadamu, unyonyaji na udhalilishaji wa watoto kingono ni muhimu sana na umekuja kwa wakati unaofaa katika nchi yetu" amesema Dkt. Ndumbaro.

Kwa msingi huo, sisi sote tuliopewa dhamana ya kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa kwa Makosa ya Biashara Haramu ya Binadamu, Ukatili na Udhalilishaji wa Watoto Kingono na Uhalifu Unaovuka Mipaka ya Nchi katika jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatuna budi kuitumia fursa hii ili kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kuhudumia taifa hili. Huu ni wakati wa kubuni mbinu mbali mbali zitakazoweza kubainisha hila na ghilba za wahalifu pia kubainisha changamoto zinazowakabili wapambanaji wa kazi hii na kutafuta mbinu muwafaka za kukabiliana nazo ili kufikia malengo tuliojiwekea.

Ubunifu wa mbinu mpya ni lazima utekelezwe sambamba na kuongeza uwezo wetu wa teknolojia ya mitandao ambayo baadhi ya wakati inatumika vibaya ili kuwanufaisha wahalifu wanaotaka mafanikio bila ya kufuata na kuheshimu sheria za ndani ya nchi na kimataifa.

" Kwa msingi huu sisi sote tuliopewa dhamana ya kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa kwa Makosa ya Biashara Haramu ya Binadamu, Ukatili na Udhalilishaji wa Watoto Kingono na Uhalifu Unaovuka Mipaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatuna budi kuitumia fursa hii ili kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kuhudumia taifa hili." Amesema Dk Ndumbaro na kusisitiza

" Huu ni wakati wa kubuni mbinu mbali mbali zitakazoweza kubainisha hila na ghilba za wahalifu pia kubainisha changamoto zinazowakabili wapambanaji wa kazi hii na kutafuta mbinu muwafaka za kukabiliana nazo ili kufikia malengo tuliojiwekea" amesisitiza.

Amesema Ubunifu wa mbinu mpya ni lazima utekelezwe sambamba na kuongeza uwezo wa teknolojia ya mitandao ambayo baadhi ya wakati inatumika vibaya ili kuwanufaisha wahalifu wanaotaka mafanikio bila ya kufuata na kuheshimu sheria za ndani ya nchi na kimataifa.

Akizungumzumzia mradi huu, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania ( DPP) Bw. Slyvester Mwakitalu amesemea mradi huo ni wa miaka minne kuanzia Desemba, 2021 hadi Desemba 2025 na unatekelezwa kwa gharama ya dola za Kimarekani 6,434,320 ambapo zitatumika kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

"Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza na Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) likishirikiana na UNICEF pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM)" amesema Mwakitalu.

Mwakitalu amesema mradi huo umelenga kujenga uwezo wa kiutendaji kwa taasisi za Serikali zinazohusika katika utekelezaji wa sheria za kupambana na uhalifu mkubwa wa kupangwa ambapo kwa Tanzania Bara utajikita zaidi katika makosa ya biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu na udhalilishaji (unyanyasaji) wa watoto.

"Lengo kuu la mradi huu wa SOC ni kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi na usalama vinavyohusika katika utekelezaji wa sheria za mapambano dhidi ya uhalifu mkubwa wa kupangwa hasa katika nyanja za upelelezi, uendeshaji wa mashtaka na ulinzi kwa wahanga na manusura" Amesema Mwakitalu.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima amesema uzinduzi wa kikosi hicho umekuja wakati muafaka wakati Serikali ikiendelea kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.