Kikosi kazi cha maboresho ya Mfumo wa CMIS
Kikosi kazi cha maboresho ya Mfumo wa CMIS
06 May, 2024

Picha ya pamoja ya Kikosi kazi kinachoshughulikia maboresho ya Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya, Kuchakata na Kutunza Kumbukumbu za Kesi za Jinai (CMIS) yanayoendelea kufanyika Jijini Dar es salaam.
Kikosi kazi hicho kinahusisha baadhi ya wataalam wa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka akiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Bw. Frank Shame, Mawakili wa Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).