Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

KAIMU MKURUGENZI ATOA WITO KWA WAKUU WA MASHTAKA WA WILAYA NA WAENDESHA MASHTAKA VIONGOZI
25 Feb, 2022
KAIMU MKURUGENZI ATOA WITO KWA WAKUU WA MASHTAKA WA WILAYA NA WAENDESHA MASHTAKA VIONGOZI

Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka ambae pia ni Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji wa Kesi Bi. Neema Mwanda amewataka Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi kwenda kuwa waalimu kwa wengine kwenye vituo vyao vya kazi ili kila mtumishi apate uelewa zaidi juu ya namna ya kuutumia mfumo huu katika majukumu yao ya kila siku kwani kazi zote zinatakuwa zinafanyika kwa njia ya mfumo na sio tena makaratasi.

"Tujaribu kujifunza huu mfumo, na tukishamaliza kujifunza tukirudi sisi ni waalimu kwa wale ambao tumewaacha kule, tunategemea mkapeleke hii elimu ambayo mmeipata kwa wengine"

Amezungumza hayo Mkurugenzi Mwanda wakati akifungua Mafunzo ya Utumiaji wa Mfumo wa Kielekitroniki wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika masuala ya Kesi kwa Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi wanaoshughulika na Takwimu yaliyoanza tarehe 22 Februari, 2022 na kumalizika tarehe 25 Februari, 2022 Jijini Dar es salaam katika ofisi za TAGLA zilizopo Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Pia Mkurugenzi Mwanda alitoa pongezi kwa Wakuu wa Mashtaka wa Wilaya na Waendesha Mashtaka Viongozi kwa utendaji wao wa kazi mzuri kwenye vituo vya kazi katika kuhakikisha Taasisi inasonga mbele.