Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

JELA MIAKA 30 KWA KULIMA, KUSAFIRISHA NA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
10 Apr, 2021
JELA MIAKA 30 KWA KULIMA, KUSAFIRISHA NA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA


Watu wawili ambao ni Damian Jankowski Kryzstof raia wa Polanda na mkewe Bi. Eliwaza Raphael Pyuza raia wa Tanzania wamehukumiwa kifungo cha miaka thelathini jela kwa makosa matatu.

Washtakiwa hao wamekutwa hatiani katika kesi Namba 79 ya mwaka 2020 na makosa ya kustawisha mimea 729 ya Bhangi, makosa mawili ya kusafirisha dawa za kulevya kilogram 15.6 na kilogram 1.6 za bhangi.

Awali ilielezwa mahamakani hapo na Mawakili wa Serikali Ignas Mwinuka, Verdiana Mlenza na Lilian Kowero kuwa washtakiwa hao walikutwa wakifanya shuguli hizo za kulima, kutumia na kusafirisha dawa za kulevya kinyume cha sheria.

Akitoa hukumu hiyo kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Moshi Mhe. Jaji B. Maziku alisema kuwa mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi toka Jamhuri ambao haukuwa na shaka na kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa hao.

Aidha katika kesi hiyo washtakiwa Eliwaza Raphael Pyuza, Hanif Hassanal Kanani raia wa Tanzania mwenye asili ya kihindi na Boniface George Kessy Mtanzania wametiwa hatiani kwa kosa la matumizi ya dawa za kulevya aina ya bhangi na kupewa adhabu ya kulipa faini ya Tshs 4,000,000/= kila mmoja au kwenda jela miaka 3.

Hata hivyo katika hukumu hiyo, mahakama imetaifisha shamba la ekari moja na nusu lililopo Himo njia panda ambalo limezungushiwa uzio wa tofali, fedha taslimu shilingi milioni 26,765,000/= alizokamatwa nazo Bw. Damian Jankowski Krzystof, simtanki 2 za lita 2000 kila moja na pikipiki kubwa moja aina ya KTM Adventure 690R yenye namba za usajili MC 972 AAD.