Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

HIFADHI YA BONDE LA KILOMBERO NI MUHIMU KWA MAISHA, ACHENI KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU DPP BISWALO
17 Feb, 2021
HIFADHI YA BONDE LA KILOMBERO NI  MUHIMU KWA MAISHA, ACHENI KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU  DPP BISWALO

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw Biswalo Mganga amewataka Wananchi wanaofanya shughuli za kilimo katika maeneo ya hifadhi kusitisha shughuli hizona kwenda kutafuta sehemu nyingine za kuendeshea shughuli zao ili kulinda mazingira.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Wilaya ya Kilombero alisema wakati wote maslahi ya Taifa yanatangulia maslahi binafsi hivyo ulinzi wa hifadhi ni jambo.muhimu katika kulinda maslahi mapana yaTaifa.

Alisema bonde la Kilombero ni eneo linalotegemewa sana katika mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere unaojengwa Rufiji Pwani hivyo uharibifu wa maliasili katika bonde hilo haukubaliki hata kidogo.

Alisema mpaka hivi sasa bado wapo watumishi wa Serikali wanaenda kulima na kufuga katika maeneo ya Bonde la mto Kilomberoninawataka waache kufanya hivyo kwa kuwa wanaharibu mazingira.

"Sitaangalia sura ya mtu, awe mbunge,mwanasiasa, kiongozi wa dini katika kulinda bonde hili.nitachukua hatua kwakuwa maslahi binafsi hayawezi kuzidi maslahi ya Watanzania Milioni Sitini." Alisisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka Mganga.

Alisema Serikali imewekeza fedha nyingi katika mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere na Bwawa hilo kwa kiasi kikubwa linategemea maji kutoka Kilombero hivyo uharibifu ukitokea halafu maji yakikosekanaTaifa litakuwa limepoteza fedha nyingi, lakini tukizembea fedha za Taifa zitakuwa zimepotea.

Aidha, alisema kuwamuendelezo wa shughuli za kilimo kwenye maeneo hayohusababisha nchi yetu itaendelea kuagiza umeme kutoka nje ya nchi, viwanda vyetu vitaendelea kukosa umeme wa uhakika.

Nikiwa mimi DPPsitaangalia sura ya mtu, Maslahi ya Mbunge au diwani tunaweka pembeni wakati wote tunatanguliza maslahi ya Taifa kwa kuwa hatuwezi kuona mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere unaharibika kwa sababu ya maslahi ya watu wachache.

NiwaombeWakuu wa Wilaya msirudi nyuma kuhakikisha mnazuia shughuli za kibinadamu katika eneo hilona kuhakikishaSheria zibafuatwa, pia wananchi wahakikishe wanatafuta maeneo mengine ya kulima. Alisisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka.