Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

DPP MWAKITALU AHITIMISHA ZIARA KATIKA MAGEREZA YA UKONGA,KEKO NA SEGEREA AHAIDI KUPELEKA MAHAKAMANI KESI ZENYE USHAHIDI.
13 Jun, 2021
DPP MWAKITALU AHITIMISHA ZIARA KATIKA MAGEREZA YA UKONGA,KEKO NA SEGEREA AHAIDI KUPELEKA MAHAKAMANI KESI ZENYE USHAHIDI.


Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Sylvester Mwakitalu amehitimisha ziara yake ya kutembeleana kukagua hali ya Magereza ya Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kutembelea na kuzungumza na Mahabusu pamoja na wafungwa walioko katika magereza yote matatu ya mkoa huo.

Akizungumza mara baada ya kujionea hali ilivyo katika Magereza hayo, baada ya kuhitimisha ziara kwa kutembelea Gereza la Mahabusu Segerea DPP Mwakitalu amesema Changamoto alizoziona ndani ya magereza hayo zitamsadia katika kufanya maamuzi na kuboreha utendaji kazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

DPP Mwakitalu alisema changamoto zilizowasilishwa na baadhi ya mahabusu walioko gereza la Segerea ambazohazipo ndani ya uwezo wa Ofisi ya Mashtaka atakahikikisha anazifikisha kwa wahusika ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi ambapo amesema maeneo yanayohitaji suluhisho la pamoja atahakikisha anakaa na wadau ili kutafuta suluhisho la pamoja.

“Kwa changamoto ambazo ziko chini ya ofisi yangu, nitazifanyia kazi kwaharaka kadri iwezekanavyo ili hakiiweze kutendeka,haya mengineambayo yako nje ya Ofisi yangu nitawashirikisha wadau wakiwemo mahakama, wapelelezi na wachunguzi ili tuwe na suluhu ya pamoja”

Aidha, DPP Mwakitalu akizugumzia chagamoto ya kuchelewa kwa upelelezi wa mashauri mbalimbali alisema kuwa wapelelezi wanaoshugulikia kesi ni wadau wake wa karibukwani bila uwepo wao yeye hawezi kufanya kazi hivyo ameahidi kukaa kwa pamojaili kesi zilizoko mahakamani ambazo upelelezi wake haujakamalika uweze kufika mwisho.

Alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka katika kutekeleza majukumu yake itaendelea kufanya kazi zake kwa kutenda haki.

Mwakitalu alisema kuwa kwa sasa Ofisi yake kwa pamoja na watendaji wataanza kazi ya kupitia upya majalada ya kesi ili kubaini kama yana ushahidi wa kutosha kesi ziendelee na kama ushahidi wake ni hafifuatayafanyia maamuzi.

“Naombaniwaeleze changamoto hizi na ushauri wenu nimeupokea kwa sasa hatuatulizonazo ni kupitia upya majalada ya kesi ili kuona lipi linafaa kuendlea a lipi linafaa kufanyiwa maamuzi upya”alisema DPP Mwakitalu

Katika hatua nyingine DPP alisema kuwa Ofisi yake kwa sasaitahikikisha inapeleka kesi mahakamani zenye ushahidi kamili na zile ambazo bado hazijapata Ushaihidi kamili hazitafikishwa Mahakamani ili kuondoa changamoto ya Msongamano Magerezani .

Kuhusiana na suala la utoaji wa vibali vya kesi DPP Mwakitalu alisema kuwa atahakikisha vibali vya Kesi(Concert)ambazo zimekwama kutokana na kukosa kibali hicho atahakikishavibali hivyo vinatolewa ili kesi ziweze kuendelea.

Aidha, DPP Mwakitalu ametembelea magareza ya Keko,Segerea na Gereza Kuu Ukonga ambapo alisema kuwa huo ni Mwendelezo wa ziara zake za kutembelea na kukagua hali ya magereza hapa nchini, kusikiliza kero na changamoto za wafungwa na mahabusu ili Ofisi yake iweze kuzitafutia Suluhu