Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

DPP AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA KUONGEZA BIDII KATIKA KAZI
02 May, 2025
DPP AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA KUONGEZA BIDII KATIKA KAZI

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  kuongeza bidii, jitihada na ubunifu katika kazi ili Ofisi hiyo iwe ni ofisi bora na pia iwe ni ofisi ambayo wananchi wanakimbilia kupata huduma na kupata haki yao.

Mkurugenzi Mwakitalu amebainisha hayo wakati alipokutana na kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka mara baada ya kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (MeiMosi) yaliyofanyika leo tarehe 1 Mei, 2025 katika viwanja vya Bombadia Mkoani Singida.

Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Mashtaka ametoa pongezi kwa watumishi hao kwa kujituma kufanya kazi vizuri na kuleta matokeo chanya katika taasisi hiyo.

"Nimepita baadhi ya mikoa na nimeona wananchi wanaamini wakija Ofisi ya Taifa ya Mashtaka watapata ufumbuzi wa matatizo yao." Ameyasema Mkurugenzi Mwakitalu