DPP AWATAKA WAAJIRIWA WAPYA KWENDA KUFANYA KAZI KWA WELEDI, UADILIFU NA UZALENDO

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Sylvester Mwakitalu amewataka watumishi wapya walioajiriwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambao ni Mawakili wa Serikali na Makatibu Sheria kwenda kufanya kazi kwa weledi, umakini, uadilifu na uaminifu pamoja na kuzingatia Sheria, Kanuni na Misingi ya Utumishi ya Umma ili kuifanya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kuendelea kuwa Taasisi yenye misingi bora na ya mstari wa mbele katika kusimamia haki.
“Kufanya kazi kama Wakili wa Serikali ni heshima kubwa sana hivyo naomba muilinde heshima hiyo kwani kazi yetu inahitaji umakini, weledi, uadilifu na uaminifu, tunataka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iendelee kuwa mstari wa mbele kwenye kusimamia haki za watu na hili tunalitegemea kutoka kwenu.’’
Mkurugenzi wa Mashtaka ameyasema hayo tarehe 5 Februari, 2025 wakati akizungumza na watumishi waajiriwa wapya waliofika Makao Makuu, Dodoma kwa ajili ya kuchukua barua zao za kwenda kuripoti katika vituo vya kazi walivyopangiwa kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Mkurugenzi Mwakitalu alisema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni ofisi ambayo imebeba haki za watu mkononi na kwamba maamuzi watakayoenda kufanya waajiriwa hao wapya ya kushtaki ama kutokushtaki ni maamuzi ambayo moja kwa moja yanagusa haki za watu, hivyo aliwaasa kuwa wanapaswa kuwa makini katika kila hatua wanayoifanya na kuhakikisha wanajiandaa vizuri kabla ya kwenda mahakamani ili kuisaidia mahakama kufanya maamuzi yaliyosahihi katika utoaji haki.
Aidha, amewataka pia waajiriwa wapya hao kutenga muda kupitia miongozo mbalimbali ambayo imewekwa katika tovuti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ambayo itawasaidia kujifunza na kuongeza uzoefu katika utendaji kazi wao wa kila siku.
”Uzoefu mlioupata huko kabla hamjaja hapa uleteni, kama kuna kitu kinaweza kutusaidia kuboresha utoaji wetu huduma kwa wananchi leteni na sisi tutakuwa tayari kupokea na kufanyia kazi kama kitaleta tija kwenye kazi zetu.”, Aliongea Mkurugenzi Mwakitalu
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka Bi. Bibiana Kileo amewapongeza waajiriwa wapya kwa kupata nafasi ya kuingia katika Utumishi wa Umma na pia kupata bahati ya kuungana na familia ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka hivyo na kuwataka kwenda kuzingatia yale yote watakayoelekezwa wakati wakiwa kazini.
‘’Mkizingatia yale yote mtakayoelezwa na viongozi wenu itawaletea mafanikio makubwa sana kwenye safari yenu ya utumishi na kukuwa katika taaluma yenu.’’ Alisema Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Simon Ntobbi amewaasa waajiriwa wapya hao kuwa na hofu ya Mungu ili waweze kutenda haki kwa wananchi watakaokwenda kuwahudumia.
‘’ Tunashukuru kwa kupata nguvu mpya hivyo mkiwa kama Mawakili tunawategemea mkatende haki, mkawasaidie wananchi wa hali ya chini naya juu kwa kutenda haki." Aliyasema hayo Mkurugenzi wa Utawala.
Katika hatua nyingine, watumishi hao wapya walipata pia fursa ya kuelekezwa Masuala mbalimbali ikiwemo miongozo na elimu kuhusa Afya Mahali Pa Kazi na uepukaji wa vitendo vya Rushwa ambapo walijaza fomu za Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na kujifunza kuhusu Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma, wasilisho lililotolewa na Afisa Tawala Mkuu, Ndugu Juma S. Katanga.