Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

DPP AWATAKA MAWAKILI WA SERIKALI NCHINI KUFUATA MAADILI KWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA
17 Mar, 2021
DPP AWATAKA MAWAKILI WA SERIKALI NCHINI KUFUATA MAADILI KWA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA RUSHWA

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga akifungua mafunzo kwa mawakili 29 wa serikali toka mikoa yote nchini juu ya kuwajengea uwezo wa Utendaji kazi.

Mashtaka wa Serikali wameaswa kufanya kazi zao kwa kufuata maadili Ili kuepusha malalamiko kutoka kwa Umma juu ya utendaji kazi wao.

Akizungumza Machi 16, 2021 Jijini Mwanza wakati akifungua mafunzo ya mawakili 39 kutoka katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mikoa na Wilaya ambapo Mkurugenzi wa Mashtaka Bw.Biswalo Mganga amesema kuwa mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo wa utendaji kazi, katika uendeshaji wa kesi za rushwa, utakatishaji fedha na udanganyifu kwa njia ya kimtandao.

Biswalo amesema Dunia ya sasa inaendana na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia hivyo lengo la kuwakutanisha mawakili hawa ni kuwajengea uwezo, kubadilishana uzoefu na wakati huo huo kujifunza mbinu mpya za kuenenda na nyakati za mabadiliko.

Bw. Mganga aliendelea kueleza kuwa Taasisi yao inaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha kuwa wanapambana kuharakisha kutatua changamoto ya makosa hayo kwa haraka ili jamii iweze kupata haki kwa wakati, na kuwezesha kufanya kazi zao za kimaendeleo kwa wakati.

Biswalo amesema Ofisi ya Taifa ya Mashtaka pamoja na Waendesha Mashtaka ina changamoto nyingi inazokabiliana nazo hivyo kuwepo kwa mafunzo ya mara kwa mara ni mhimu kwa watendaji hao.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Suleiman Nyakulinga amesema kutokana na ongezeko la changamoto ya uhalifu wa kimtandao mafunzo ya mara kwa mara kwa watendaji hao itawasaidia kufahamu namna nzuri ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Nyakulinga ameeleza kuwa makosa ya Utakatishaji Fedha na Uhalifu wa Kimtandao yameongezeka hivyo kuwa na Waendesha Mashtaka wenye uelewa mkubwa ni mhimu kwa wakati huu.

Naye Wakili wa Serikali toka Mkoani Arusha ambaye amehudhuria mafunzo hayo Bw. Tusaje Samwel amesema kutokana na changamoto zinazojitokeza katika nyanja ya makosa hayo ni mhimu kwao kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo ili kuwawezesha kukabiliana na makosa mbalimbali ya kiuhalifu.