Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

DPP AFUNGUA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA
11 Mar, 2024
DPP AFUNGUA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

[13:18, 10/03/2024] 568221: Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu amefungua  Kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kinachofanyika tarehe 10 hadi 11 Machi, 2024 Mkoani Pwani.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mashtaka amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwani kinalenga kukumbushana,  kujadiliana na kupanga maazimio mbalimbali yatakayowezesha utekelezaji wa majukumu yao kuwa rahisi ili kuweza  kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia.

"Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni ofisi nyeti kwa maana tunatoa huduma na kugusa haki za wananchi, maamuzi yetu yanakwenda kugusa haki za watu, tusipokuwa makini na kufanya kazi hii kwa weledi na kwa uaminifu kuna watu tutawaumiza." Amefafanua hayo Mkurugenzi Mwakitalu.

Pia Mkurugenzi wa Mashtaka ameeleza kuwa kupitia kikao kazi hicho watajadiliana na kutafuta suluhu yale maeneo ambayo yamebeba changamoto nyingi zaidi, na maazimio yatakayotolewa na kukubaliana kupitia kikao hicho yazingatiwe na kutelezwa kwa wakati.

"Tuzitumie siku mbili hizi vizuri ili tuweze kujadiliana na tutoke na maazimio ya pamoja, na kwa kufanya hivyo basi tutaendelea kuimairisha ofisi yetu na utoaji wetu wa huduma kwa watu ambao tumepewa jukumu la kuwahudumia." Ameyasema hayo DPP

Sambamba na hilo Mkurugenzi wa Mashtaka amewasisitiza watumishi ambao wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki wa Manunuzi ya Umma (NEST) kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zilizowekwa na kufanya manunuzi yale ambayo yatasaidia katika kuimairisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Tunatumia fedha za umma na fedha hizi lazima zitumike kwa utaratibu na kwa miongozo ya fedha za umma iliyopo." Amebainisha hayo Mkurugenzi Mwakitalu.
[13:19, 10/03/2024] 568221: Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Bw. Sylvester Mwakitalu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kinachofanyika tarehe 10 hadi 11 Machi, 2024 Mkoani Pwani.