Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA

AHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA.
07 Mar, 2025
AHUKUMIWA  MIAKA 30 JELA KWA  KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA.

Mahakama ya Wilaya ya Momba imemuhukumu Bw. Laurent Emmanuel Sigula (18) kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia kusafirisha dawa za kulevya aina bhangi yenye ujazo wa gramu 240.

Hukumu hiyo imetolewa tarehe 6 Machi, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu Raymond Kaswaga baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa kutoka upande wa mashtaka. 

Mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 24 Aprili, 2024 katika  eneo la Migombani, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba alipokutwa na Mtendaji wa Mtaa akimiliki misokoto 122 ya bhangi yenye gramu 240 kisha kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi na alipohojiwa alikiri bhangi hiyo kukutwa nyumbani kwake.

 Kesi hii iliendeshwa na Mawakili wa Serikali wawili kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka akiongozwa na Wakili Shadrack  Meli akisaidiana na Sadam Kitembe.