Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

NATIONAL PROSECUTIONS SERVICES

Ahukumiwa kwenda jela kwa kosa la kukutwa na Nyara za Serikali
15 Sep, 2020
Ahukumiwa kwenda jela kwa kosa la kukutwa na Nyara za Serikali

Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara katika kesi ya Uhujumu Uchumi Na. 20/2020 imemuhukumu kwenda jela miaka ishirini mshtakiwa Athuman Rajabu Ramadhani kwa kosa la kukutwa na Nyara za Serikali ambazo nyama ya Pundamilia yenye thamani ya Tsh 2,760,000/ na vipande 5 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Tsh. 34,500,000/ kinyume cha kifungu cha 86(1),2(b) cha Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kikisomwa pamoja na Aya ya 14 ya jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi sura ya 200 marejeo ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 26 August mwaka 2019 katika kijiji cha Magugu kilichopo Babati, Manyara

Mshtakiwa ana umri wa miaka 29 na Mkazi wa Kijiji cha Magugu kilichopo Babati Manyara.

Katika kesi hiyo upande wa Mashtaka uliwasilisha mahakamani mashahidi 4 na vielelezo 8 na upande wa utetezi alikuwa shahidi mmoja.

Mshtakiwa amepatikana na hatia na Mahakama imemwamuru kutumikia kifungo cha miaka ishirini jela na kielelezo alichokutwa nacho kutaifishwa na kuwekwa chini ya uangalizi wa Mkurugenzi wa Maliasili.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa tarehe 06 Septemba 2019 na hukumu imetolewa tarehe 14 September, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Babati Mhe. Victor Kimario ambapo upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Timotheo Mmari na mwendesha Mashtaka wa TANAPA Rasticus Mahundi.